Jina la Kiswahili linadokeza imani ya kale ya kwamba chunusi ilitokana na kijana kutunukwa (kutokea kupendwa) na mwingine. Kumbe maelezo ya sayansi ni kama ifuatavyo.
Jeni zinakadiriwa kusababisha asilimia 80 za visa hivyo.[2] Si dhahiri kama lishe husababisha hali hii.[2] Hakuna ushahidi wa manufaa ya usafi wala miale ya jua.[2]
Hata hivyo uvutaji sigara huongeza hatari ya kupata chunusi na kuzidisha ukali wake.[5]
Kuna njia nyingi za matibabu za kupunguza chunusi zikijumuisha kubadili hali ya maisha, taratibu na dawa. Kula kabohidrati chache na zinazomeng’enywa kwa urahisi, kama vile sukari, kunaweza kusaidia.[8]
Matibabu ya mapema na hima hupendekezwa na baadhi ya watu ili kupunguza athari jumla za muda mrefu.[4] Pia limau na asali ni dawa nzuri kwa kutoa chunusi na madoa meusi [11].
Uenezi
Chunusi mara nyingi hutokea katika ubalehe huku ikiathiri takriban asilimia 80–90 ya vijana katika nchi za Magharibi.[12][13][14] Viwango vya chini huripotiwa katika baadhi ya jamii za mashambani.[14][15]
Katika mwaka wa 2010, chunusi ilikadiriwa kuathiri watu milioni 650 duniani kote, hivyo kuufanya kuwa ugonjwa wa 8 unaotokea mara nyingi zaidi ulimwenguni.[16]
Watu pia wanaweza kuathiriwa kabla na baada ya kubalehe.[17] Ingawa hali hii haitokei mara nyingi kwa watu wazima ikilinganishwa na vijana, takriban nusu ya watu katika umri wa miaka ya ishirini na ya thelathini huendelea kuwa na chunusi.[2]
Marejeo
↑Adityan B, Kumari R, ThappaDM (Mei 2009). "Scoring systems in acne vulgaris". Indian Journal of Dermatology, Venereology and Leprology. 75 (3): 323–6. doi:10.4103/0378-6323.51258. PMID19439902.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link) CS1 maint: unflagged free DOI (link)
↑Barnes LE, Levender MM, Fleischer AB Jr, Feldman SR (Aprili 2012). "Quality of life measures for acne patients". Dermatologic Clinics. 30 (2): 293–300. doi:10.1016/j.det.2011.11.001. PMID22284143.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link)
↑Knutsen-Larson S, Dawson AL, Dunnick CA, DellavalleRP (Januari 2012). "Acne vulgaris: pathogenesis, treatment, and needs assessment". Dermatologic Clinics. 30 (1): 99–106. doi:10.1016/j.det.2011.09.001. PMID22117871.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link)
↑Benner N, Sammons D (Septemba 2013). "Overview of the treatment of acne vulgaris". Osteopathic Family Physician. 5 (5): 185–90. doi:10.1016/j.osfp.2013.03.003.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
↑Mahmood SN, Bowe WP (Aprili 2014). "Diet and acne update: carbohydrates emerge as the main culprit". Journal of drugs in dermatology: JDD. 13 (4): 428–35. PMID24719062.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
↑Beylot, C; Auffret, N; Poli, F; Claudel, JP; Leccia, MT; Del Giudice, P; Dreno, B (Machi 2014). "Propionibacterium acnes: an update on its role in the pathogenesis of acne". Journal of the European Academy of Dermatology and Venereology : JEADV. 28 (3): 271–8. doi:10.1111/jdv.12224. PMID23905540.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
↑Chukua limao kamao kamua yale maji yake alafu jipake kwa kutumia pamba au vidole sehemu zenye chunusi au madoa ndan ya dakika kumi na tano kisha osha uso kwa maji safi na sabuni. Na ukitumia asali jipake kila siku asubuhi na usiku kabla hujalala pia limao asubuhi na usiku kabla hujalala
↑Taylor, Marisa; Gonzalez, Maria; Porter, Rebecca (Mei–Juni 2011). "Pathways to inflammation: acne pathophysiology". European Journal of Dermatology. 21 (3): 323–33. doi:10.1684/ejd.2011.1357. PMID21609898.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
↑Hay, RJ; Johns, NE; Williams, HC; Bolliger, IW; Dellavalle, RP; Margolis, DJ; Marks, R; Naldi, L; Weinstock, MA; Wulf, SK; Michaud, C; J L Murray, C; Naghavi, M (Oktoba 2013). "The Global Burden of Skin Disease in 2010: An Analysis of the Prevalence and Impact of Skin Conditions". The Journal of investigative dermatology. 134 (6): 1527–34. doi:10.1038/jid.2013.446. PMID24166134.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link)
↑Admani S, Barrio VR (Novemba 2013). "Evaluation and treatment of acne from infancy to preadolescence". Dermatologic therapy. 26 (6): 462–6. doi:10.1111/dth.12108. PMID24552409.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chunusi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.