Chuo KikuuChuo Kikuu ni taasisi ya elimu ya ngazi ya juu ambako wanafunzi wanafundishwa na wataalamu wa fani mbalimbali ambao hufundisha pamoja na kuendesha uchunguzi wa elimu mpya. Wanafunzi husoma kwenye chuo kikuu kwa shabaha ya kupata elimu hadi kupita mitihani ya shahada au digrii kama vile ya bachelor (ya kwanza), ya uzamili (master) (ya pili) na ya uzamivu, PhD (ya tatu). Sifa za Chuo kikuuSiku hizi chuo kikuu kinatakiwa kuwa na sifa kadhaa za kukitofautisha na vyuo au taasisi nyingine kama vile:
Historia ya vyuo vikuuJamii katika tamaduni mbalimbali zilianzisha taasisi maalumu kwa elimu ya ngazi ya juu. Kati ya vyuo vya kwanza vinayofanana kiasi na chuo kikuu cha kisasa kuna hasa taasisi katika Uhindi, Ugiriki ya Kale, Uajemi, Ulaya na nchi za Kiislamu. Mfumo wa kufundisha na kuratibu elimu ulio msingi wa vyuo vikuu vya kisasa ulianza hasa katika Ulaya ya karne za kati. Vyuo hivi vya Ulaya viliendelea kuwa mahali pa maendeleo na kukuza sayansi ya kisasa. Kutoka hapa mfumo wa chuo kikuu pamoja na utaratibu wa ngazi zake za elimu ulisambaa kote duniani. Vyuo vikuu vya AfrikaKitovu cha kwanza cha elimu ya hali ya juu barani Afrika kilikuwa maktaba ya Aleksandria nchini Misri lakini ilikuwa taasisi ya kukusanya vitabu na mahali pa uchunguzi, si mafundisho. Kihistoria vyuo vya kwanza vilivyotoa mafundisho kwenye hali ya juu ya kimataifa ya wakati wake vilikuwa chuo cha Al-Karaouine mjini Fes, Moroko tangu mwaka 859 BK na Al Azhar mjini Kairo, Misri tangu mwaka 975. Upande wa kusini kwa Sahara ni Madrasa ya Sankore mjini Timbuktu (Mali) iliyotoa mafundisho ya hali ya juu kuanzia takriban mwaka 1400. Vyuo vikuu vya kisasa vilianzishwa na wamisionari katika karne ya 19 nchini Sierra Leone na Afrika Kusini; vilianzishwa kama vyuo vya ualimu na kuendelea kuwa vyuo vikuu kamili. Chuo Kikuu cha kwanza katika Afrika ya Mashariki kilikuwa Chuo Kikuu cha Makerere ambacho ni chuo mama cha vyuo vya Nairobi na Dar es Salaam. Vyuo vikuu bora barani AfrikaSiku hizi ni hasa vyuo vikuu vya Afrika Kusini vinavyothaminiwa kuwa bora katika bara la Afrika. Orodha ya utathmini wa vyuo vikuu bora barani Afrika kwa mwaka 2013 ilikuwa kama ifuatayo:
Kufikia mwaka 2016, vyuo vikuu kumi bora ni vyote vya Afrika Kusini. Cha Dar es Salaam kimekuwa cha 26.[1] Majereo |