Conrad George Rutangantevyi
Conrad George Rutangantevyi (alizaliwa 26 Januari 1991), ni msanii chipukizi wa hip hop na Bongo Flava nchini Tanzania. Alizaliwa Kanazi, wilaya ya Ngara, mkoa wa Kagera, kaskazini-magharibi mwa Tanzania. Amesoma shule ya msingi Kanazi kuanzia mwaka 2000 hadi 2006, akiwa darasa la tano kwa mara ya kwanza alishiriki mashindano yaliyoandaliwa na Radio kwizera iliyopo mjini Ngara kwa ushirikiano wa shirika la kuhudumia watoto duniani UNICEF, lilofanyika wilayani Ngara mwaka 2005, ambapo Conrad George Rutangantevyi (Conidee) alishiriki kama mwanahip hop hata hivyo katika mashindano haya Conidee alishika nafasi ya nne katika mashindano hayo,Kuanzia hapo ndipo mwanzo wa safari ya muziki ukaanza. Mwaka 2007 alianza kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Rulenge, kutokana na sababu za kisanaa aliahamishwa shule mwaka 2009 akiwa kidato cha tatu,April 2009 hadi 2010 alisoma katika shule ya sekondary Bishopmpango, ambako alianzisha 2C2PANE kundi la muziki ,ambalo lilidumu kwa mda wa miaka miwili na kusambaratika baada ya kuhitimu masomo ya kidato cha nne mwaka 2010.Mwaka 2011 alijiunga na shule ya Sekondari kuu Lukole ambako aliweza kusimama kama mwimbaji asiye na kundi, mwaka 2013 baada ya kuhitimu kidato cha sita kabla ya kujiunga na elimu ya juu ametamba na nyimbo kama Takataka, na kutangaza kuachia albamu yake ya kwanza maarufu kama B29, ambao ndio wimbo ambao unamtambulisha kwa sasa kama chipukizi.
|