DolaDola (kutoka Ar. دولة daulat; nchi, serikali, taifa; ing. state) ni utaratibu wa kisiasa wa jamii katika eneo fulani. Ufafanuzi wa "Dola"Fani mbalimbali huwa na maelezo tofauti kiasi juu ya maana ya dola:
Aina za DolaDola hutokea kwa maumbo mbalimbali kwa mfano jamhuri au ufalme. Dola inaweza kujitegemea kabisa au kuwa sehemu ya shirikisho au muungano kama Muungano wa Madola ya Amerika. Ndani ya maumbo haya kuna njia mbalimbali za kutekeleza mamlaka na kuratibu serikali kwa mfano kwa njia ya demokrasia au udikteta. Vyombo vya DolaKiini cha dola ni utekelezaji wa mamlaka katika eneo fulani. Hapo kuna chombo kinachoitwa serikali chenye mamlaka haya mkononi. Serikali inaangaliwa na taasisi nyingine. Katika madola ya kisasa kuna mgawanyo wa madaraka wa dola kwa taasisi mbalimbali:
VYombo vingine ni matawi mbalimbali ya serikali kulingana na katiba ya dola. Tazama piaMarejeo |