Fredinah Peyton
Fredinah Peyton (anajulikana na Watanzania wengi kwa jina la Rah P ambalo limetokana na herufi chache za jina lake) ni mwanamuziki wa Rap na Hip Hop kutoka nchini Tanzania. Rah P alizaliwa mwaka 1986 mkoani Shinyanga akiwa mtoto wa pili kati ya watoto wanne wa mzee Peyton, akiwa amepatia elimu yake ya msingi nchini Kenya na kuhitimu kidato cha nne huko nchini Uganda, na kuendelea na A level huko huko nchini Uganda. Maisha ya MuzikiMwanadada huyu asiyekuwa na historia kubwa katika ulimwengu wa muziki alianza kuimba baada ya kuwa mpenzi mkubwa wa wanamuziki wa kutoka nchini Marekani kama vile akina Mc Lyte,Queen Pen na Destiny Child, mara nyingi alikuwa akiigiza nyimbo za wanadada hawa na kuzicheza kwenye matamasha mbalimbali ya kishule jambo lililomuongezea umaarufu mkubwa huku mama yake mzazi akipinga vikali kitendo cha mwanae kujishughulisha na muziki akiwa shuleni lakini wakati huohuo akipata msukumo kutoka kwa Dada yake mkubwa Georgia. Mwaka 2003 mwanzoni nyota ya kuwa mwanamuziki ilianza kung’ara baada ya kupata nafasi ya kuimba kwenye tamasha moja huko Butiama,Shinyanga huku kukiwa na Wanamuziki wengine kama wakina Mr Nice na Benjamin wa Mambo Jambo waliokuwa ziarani mkoani humo, baada ya hapo ndipo mama yake alipoanza kumruhusu kufanya muziki ila kwa masharti ya kumaliza shule kwanza au kufanya wakati wa kipindi cha likizo
|