Haki za binadamuKwa orodha za haki za binadamu angalia makala Tangazo kilimwengu la haki za binadamu Haki za binadamu ni wazo la kuwa kila mtu anastahili haki kadhaa si kwa kutegemea cheo, wala taifa, wala tabaka, wala jinsia, wala dini kwa sababu tu yeye amezaliwa binadamu. Haki hizi zimeorodheshwa hasa katika Azimio la Kimataifa juu ya Haki za Binadamu lililotolewa na Umoja wa Mataifa mwaka 1948. Tamko la UM lilikuwa kamilisho la majadiliano kuhusu haki hizi yaliyoendelea kwa karne kadhaa. Hoja la kimsingi ni kwamba, "Watu wote wamezaliwa huru; hadhi na haki zao ni sawa. Wote wamejaliwa akili na dhamiri, hivyo yawapasa watendeane kindugu". (Kifungu 1 cha tangazo la 1948). Mizizi ya haki hizo inapatikana katika falsafa na dini mbalimbali ya tangu kale, lakini ilikuwa wakati wa zama za mwangaza tangu karne ya 18 ya kwamba haki hizi zilijadiliwa kwa undani pamoja na swali: ni matokeo gani kuwepo kwa haki hizi yanaleta kwa utaratibu wa siasa, serikali na jamii. Mfano wa haki za kimsingiHaki za binadamu za kimsingi ni pamoja na:
Kwa mengine angalia makala juu ya tangazo kilimwengu la haki za binadamu. Viungo vya NjeShirika zinazopigania haki za binadamu
|