Hugo Wallace Weaving (amezaliwa tar. 4 Aprili1960, Nigeria) ni mwigizaji filamu wa Kiingereza, vilevile mwigizaji wa sauti yaani kama kuigiza sauti ya katuni au sauti za kirobot. Huenda akawa anafahamika kwa jina la Agent Smith kutoka katika mfululozo wa filamu za Matrix.
Wasifu
Maisha ya awali
Weaving alizaliwa nchini Nigeria na wazazi wa Kiingereza Anne, aliyekuwa mwongozaji wa watalii, na Wallace Weaving, mwanaseismolojia (mstadi wa maafa asilia ya dunia). Hugo utoto wake wote aliutumia akiwa nchini Afrika Kusini na baadae familia ikarudi Uingereza, wakati Hugo bado yungali bwana mdogo. Akiwa Uingereza akapelekwa shule ya bweni na ilipofika mwaka 1976 akaelekea Sydney nchini Australia, akiwa huko akajiunga na shule moja hivi iliokuwa inafundisha maswala ya lugha. Shule ilikuwa naongozwa na muunganiko wa baadhi ya makanisa. Baada ya hapo akajiunga tena na taasisi ya sanaa na maigizo (National Institute of Dramatic Art) ya nchini Australia na kumaliza mnamo mwaka wa 1981.
Filamu alizoigiza
Maybe This Time (1980), kama Mwanafunzi wa 2
The City's Edge (1983), kama Andy White
"Bodyline" (1984), kama Douglas Jardine
For Love Alone (1986), kama Johnathan Crow
"Melba" (1987), kama Charles Armstrong
The Right Hand Man (1987), kama Ned Devine
Dadah Is Death (1988), kama Geoffrey Chambers
"The Dirtwater Dynkamaty" (1988), kama Richard Ekamatwick
"Bangkok Hilton" (1989), kama Richard Carlisle
...Almost (1990), kama Jake
[Proof (1991), kama Martin
Road to Alice (1992), kama Morris
Frauds (1993), kama Jonathan Wheats
Reckless Kelly (1993), kama Sir John
The Custodian (1993), kama Det. Church
"Seven Deadly Sins" (1993), kama Lust
Exile (1994), kama Innes
The Adventures of Priscilla, Queen of the Desert (1994), kama Anthony 'Tick' Belrose/Mitzi Del Bra
What's Going On, Frank? (1994), kama Strange Packer in Supermarket
"Bordertown" (1995), kama Kenneth Pearson
Babe (1995) kama sauti ya Rex the Male Sheepdog
"Naked: Stories of Men" - Episode "Coral Island" (1996) kama Martin Furlong
"The Bite" (1996), kama Jack Shannon
True Love and Chaos (1997) kama Morris
Halifax f.p: Isn't It Romantic (1997), kama Det. Sgt. Tom Hurkos
"Frontier" (1997), kama Governor Arthur
Babe: Pig in the City (1998), kama sauti ya Rex the Male Sheepdog