Juba (mto)
0°14′58″S 42°37′51″E / 0.2495°S 42.6307°E Juba (pia: Jubba, Giuba, Ganane au Genale; kwa Kisomali Wabiga Jubba) ni mto mkubwa wa Somalia wenye maji mwaka wote. Chanzo chake ni katika nyanda za juu za Ethiopia. Unaanzia karibu na mpaka wa Ethiopia, ambao Mto Dawa na mto Ganale Dorya inaungana, halafu unatiririkia kusini moja kwa moja hadi Bahari ya Hindi karibu na mji wa Kismayu, Somalia Kusini. Wakati wa ukoloni mto Juba ulikuwa mpaka kati ya Kenya na eneo la Somalia lililokuwa chini ya Italia. Mwaka 1925 Uingereza iliwaachia Waitalia eneo la nchi kusini mwa mto (kwa Kiitalia: Territorio dell'Oltre Giuba - kwa Kiingereza: Jubaland). Kila baada ya miaka kadhaa bonde la Juba huona mafuriko. Mafuriko mabaya yaliyoleta uharibifu mwingi yalitokea mwaka 1997. Tazama piaTanbihiViungo vya nje
|