Karne ya 14Lango la Historia | Lango la Biografia | Karibuni | Orodha ya Miaka ◄ |
Karne ya 12 |
Karne ya 13 |
Karne ya 14
| Karne ya 15
| Karne ya 16
| ►
Kama kila "karne" ni kipindi kinachohesabiwa kwa hiari ya kibinadamu kwa sababu ni mgawanyo wa kalenda tu - hali halisi maendeleo na mabadiiliko makubwa hayafuati migawanyo ya kalenda ya kibinadamu. Kuna mambo mengi yaliyotokea wakati wa karne hii. Watu na matukioKarne ya saa za kwanzaLabda badiliko kubwa lilikuwa uenezi wa saa za kimekanika kwenye minara ya miji ya Ulaya. Tofauti na saa za jua au saa za maji ziliwaonyesha watu wengi wakati tena bila ya kutegemea hali ya hewa. Wataalamu wengi huamini ya kwamba hakuna mitambo mingine iliyobadilisha utamaduni wa binadamu kuliko saa. Karne ya kifo katika UlayaUlaya iliathiriwa mara ya kwanza na ugonjwa wa kuambukiza wa tauni. Tauni iliua wakulima wengi ikasababisha njaa kali; zote pamoja zikaua zaidi ya theluthi ya wakazi wote wa Ulaya. Vifo vingi vilisababisha hofu kubwa kati ya watu. Wayahudi walishtakiwa kuwa sababu ya maradhi na vifo wakauawa na kudhulumiwa katika nchi nyingi za Ulaya. Uenezaji wa milki ya Waturuki WaosmaniUdhaifu wa Ulaya katika karne hii ilisaidia uenezaji wa milki ya Waturuki Waosmani kutoka Anatolia kujiandaa kuingia nchi za Balkani (Ulaya ya Kusini-Mashariki). Hivyo utawala wa Kiislamu ulielekea kuenea hata katika mashariki ya Ulaya utakaokuwepo kwa karne tano zilizofuata. Baadaye athira yake ilifikia pwani za Uswahilini na Uganda. Milki za AfrikaKatika Afrika ya Magharibi Wahaussa wanaunda milki zao za kwanza. Mali inapanuka. Majengo makubwa ya Zimbabwe Kuu yanaanzishwa. |