KochaKatika michezo, kocha (kutoka Kiingereza: coach) ni mtu mwenye majukumu ya kuelekeza, kufundisha na kusimamia masuala yote yahusuyo mbinu na njia za uchezaji kwa timu nzima na mchezaji mmojammoja. Kocha anaweza kuwa mwalimu pia. HistoriaNeno ‘’kocha’’ limetokana na neno la Kiingereza coach, neno lililotokana na gari la kukokota la farasi lililotumika kwa mara ya kwanza nchini Hungary mji wa Kocs. Katika karne ya 19, wanafunzi katika chuo kikuu cha Oxford walitumia neno hilo kuita wakufunzi binafsi waliofundisha wanafunzi wenye uwezo mdogo wa kimasomo kufaulu katika mitihani yao, walisema kua wakufunzi hao waliwavuta wanafunzi mfano wa farasi anavyokokota gari hilo. Karne hiyo hiyo ya 19, Uingereza ilishika hatamu katika kukuza michezo. Ili mchezo uwe wa kitaalamu, ililazimu kocha awepo. Kazi hii ilidumishwa Zaidi mwaka 1994 katika enzi za Victoria. Katika vita vya kwanza vya dunia, vikosi vya kijeshi vilikuwa na makocha wa kusimamia ukakamavu wa kimwili na kujenga morali kwa wanajeshi.[1] WasaidiziKocha, hasa hasa kwenye ligi rasmi huwa na wasaidizi mmoja au zaidi pamoja na wafanyakazi wengine. Wafanyakazi hawa hujumuisha waratibu, wataalamu wa ukakamavu na usawa na wakufunzi wengine. Katika michezo ya nguvu, majukumu ya wataalamu wa lishe, wanabayolojia na wataalamu wa mwili ni muhimu katika mafanikio ya kocha pamoja na mchezaji. Kwa ujumla wanafanya kazi kulenga majukumu ya mchezaji. Mpira wa Miguu “Soka”Katika soka, majukumu ya kocha hutofautiana kulingana na kiwango cha ufundishaji nan chi wanapofundishia. Katika soka la vijana wa umri mdogo, jukumu la kocha ni kusaidua vijana kukuza kiwango cha uchezaji wakisisitiza kufurahia na kucheza kwa usawa, kwa ngazi hioi mafunzo na mazoezi ya ukakamavu wa mwili na mbinu za kiuchezaji sio za muhimu sana.[2] Katika miaka ya hivi karibuni, {When|date=May 2017}} nguvu nyingi zimeelekezwa kugeuza mbinu za ufundishaji kwa vijana wa umri mdogo, mafunzo yanapaswa kuelekeza wachezaji juu ya kukuza uwezo wao zaidi na sio kushinda mashindano. Katika mchezo wa mpira wa miguu, jukumu la kocha au mkufunzi linalenga zaidi katika kufundisha na kukuza “timu ya kwanza” ya klabu. Kocha mkuu huwa na wakufunzi wasaidizi, mmoja wao akiwa na jukumu la kufundisha walinda lango. Kocha ana wasaidizi wa huduma ya kwanza pia. Mipango ya muda mrefu ya timu, ikijumuisha uhamisho wa wachezaji, kukuza vijana na huudma nyingine za kimichezo sio jukumu la kocha. Uwepo wa mkurugenzi katika timu ulianzishwa ili kuhamishia majukumu ya maendeleo na mipango ya muda mrefu ya timu kutoka kwa kocha kwenda kwa mkurugenzi, lengo likiwa ni kumpa kocha muda mwingi wa kufundisha wachezaji waliopo chini yake.[3] Mfumo huu husaidia pia kupunguza matumizi makubwa ya fedha kwa wachezaji katika kutafuta mafanikio ya haraka. Katika soka, cheo kinachotumika zaidi ni meneja, cheo hichi kinajumuisha majukumu ya kocha na mkurugenzi wa timu. BaseballKatika baseball, anagalau ngazi ya michezo rasmi Marekani ya kaskazini, mwenye majukumu ya kusimamia kazi za ukocha hatumii jina la “kocha mkuu” bali huitwa meneja. Makocha wa Baseball ni wanachama wa kikundi cha uongozi cha timu ambamo kila kocha ana kazi yake binafsi katika timu. Meneja wa base ball ana cheo sawa na kocha mkuu katika michezo mingine; Uhamisho wa mchezaji yeyote unafanyika chini ya meneja. Mara nyingi neno “meneja” linatumika kumaanisha msimamizi wa michezo, mkuu wa timu huwa anatambulika kwa jina la meneja mkuu (GM). Katika ngazi ya michezo isiyo ya malipo, neno meneja ni sawa na kocha wa michezo mingine. Mtu anayefahamika kwa jina la meneja katika ngazi ya michezo ya kulipwa ni sawa a kocha mkuu katika michezo ya kujitolea hasa hasa mashindano ya vyuo vikuu nchini Marekani. American footballKatika mchezo maarufu kwa jina la American football wenye asili ya Marekani, idadi ya makocha na makocha wasaidizi ni wengi sana. Mchezo huu unajumuisha kocha mkuu, kocha mkuu msaidizi, mratibu wa ushambuliaji, mratibu wa wazuizi, mratibu wa kikosi maalumu, kocha wa washambuliaji na walinzi wa pembeni, kocha wa kila nafasi, na kocha wa nguvu na hali ya timu.[4] UingerezaKocha wa michezo nchini Uingereza hufuata kanuni na taratibu za hali ya juu lakini inajumuisha watu wengi wanaojitolea. Ili kutambua michango ya makocha katika kuongeza idadi ya washiri katika michezo, kila baraza la michezo nchini Uingereza ina mikakati ya ufundishaji inayoambatana na mikakati ya michezo kiujumla. Mnamo mwezi Juni 2008, baraza la michezo na bodi kuu ya michezo Uingereza (NGBs) Ilipitisha mfumo wa ukocha kwa nchi ya Uingereza katika kilele cha mkutano huko Coventry. Zaidi ya michezo ipatayo thelathini huwa na program maalumu kwa ajili ya mafunzo kwa makocha wao, lengo likiwa ni kuhakikisha makocha hua na taaluma inayotambulika na shirika la (UKCC), hii ikiwa kama alama ya kuhakikisha huduma bora inatolewa na makocha hao. Kwa ujumla, mafunzo hayo huwatenga makocha katika ngazi nne tofauti, ngazi ya pili ikiwa ndio ngazi ya chini zaidi kwa kocha kufanya kazi bila msimamizi. Mafunzo ya ukocha hupangwa na kuratibiwa na bodi ya NGBs, ila hutolewa na watu wa ndani wa kujitolea. Mtu nyoyote mwenye nia ya kua kocha wa mchezo wowote, tovuti ya NGB inatoa njia ya mawasiliano ya urahisi zaidi. Hisia katika kufundisha“Hisia zinaweza kuelezewa kama sehemu tatanishi zinazoingiliana pamoja na mambo ya ndani na sababu za msingi zinazojumuisha vipengele vya utambuzi, ufumbuzi, uhusiano na mwili” (Mwenendo wa Utafiti wa Mawasiliano, 2005). Bila hisia, mawasiliano yatakua na vikwazo vingi. Hisia hutoa mazingira na sababu ya jinsi watu wanahisi baada ya hali fulani inayohusiana na mawasiliano. “Hisia zinaweza kuchukua jukumu muhimu sana jinsi tunavyofikiria na kuishi.”[5] Maamuzi hufanywa kutokana na hisia na hisia zinaweza kuonyesha moja kwa moja uzoefu katika mawasiliano. Matumaini hutokana na hisia za kibinadamu za faraja na usalama. Mhemko wa tumaini ni wakati mtu anaamini katika kitu ambacho bado hawezi kuamua. Kwa mfano, kocha anaweza kuwa na tumaini kwa wachezaji wake kwamba watacheza kwa uwezo wao wote. Mchezaji naye anaweza kupata hisia za matumaini, Mchezaji anaweza kuwa na matumaini ya ushindi akilinganisha na hali nyao ya baadae. Matumaini ni hisia ambayo inaelezea matamanio ya mtu binafsi kwa juhudi za baadaye. Matumaini ya kocha kwa timu yake ina athari chanya juu ya maendeleo na mafanikio ya timu. Ufahari ni aina ya hisia ambapo mtu hujhisi ukamilifu na mwenye furaha. Ufahari huja baada ya aina Fulani ya mafanikio. Hisia ya fahari huja baada ya kukamilisha jambo fulani. Kocha anaweza jiskia fahari kwa pekee au na wachezaji wake baada ya ushindi wa mchezo muhimu. Katika ukocha, kuwa na ufahari ni kwenye mafanikio ya timu zaidi ya mafanikio binafsi ya kocha. Ufahari kama hisia inaweza kuelezewa kama jambo muhimu katika kufanikisha mikakati ya kocha. Uhamasishaji ni aina mojawapo ya mhemko inayoelezea hisia za kutaka kufanya vizuri zaidi. Uhamasishaji mara nyingi huja baada ya mafanikio makubwa. Kwa mfano, baada ya mafanikio makubwa katika msimu, timu itajihamasisha kufanya vizuri zaidi kwa msimu unaofuata. Kocha anaweza kuhamasishwa na wachezaji wake kwasababu ya changamoto wanazompa ili naye awe vizuri zaidi. Jukumu la msingi la kocha ni kuizingatia mafanikio ya timu. Ili kocha awe na mafanikio zaidi, inampasa kuwatia hamasa wachezaji wake wawe bora. MaandaliziSemina na mafunzo ya ukocha yapo kila mahali na huongezeka kadiri ya muda. Jukumu mojawapo la kocha hasahasa kocha wa vijana ni kuhakikisha usalama kwa wanamichezo wadogo wanaosoma. Hii inahitaji ujuzi wa ufufuaji wa moyo na mishipa (CPR), jinsi nya kuzuia upungufu wa maji mwilini, na njia za kufuata mshituko wa ubongo ukimpata mchezaji.[6][7] Mikakati ya MichezoKocha mara zote ndie anayepanga mkakati wa mchezo, au maelekezo kwa wachezaji kuhusu mambo ya kufanya wakati wa mchezo. Kila mchezo hua na mkakati tofauti na wa kipekee.[8] Mfano mzuri ni katika soka, kocha anaweza kuamua awe na mlinda lango, walinzi wanne, viungo wanne, na washambiliaji wawili. Vilevile anaweza kuamua awe na mlinda lango, walinzi wane, viungo watatu na washambuliaji watatu. Maamuzi ni ya kocha katika kuamua wachezaji wangapi wacheze katika nafasi gani bila kuvunja sharia ya idadi ya wachezaji wanaohitajika kisheria. Ni majukumu ya kocha kujua muda gani na nafasi gani mchezaji Fulani acheze. Marejeo
|