M
M ni herufi ya 13 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Mi ya alfabeti ya Kigiriki. Maana za M
Historia ya alama M
Asili ya herufi M ni katika miandiko iliyotangulia alfabeti ya Kilatini. Waroma walipokea mwandiko kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki waliipokea kutoka Wafinisia. Wafinisia walikuwa na alama ya "Mem" iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya maji wakitumia alama tu kwa sauti ya "m" na kuiita kwa neno lao kwa maji "mem". Kwa kurahisisha kazi ya kuandika waliongeza mstari mrefu upande walipoanza kuandika. Wagiriki walichukua alama hiyo na kuiita "Mi" bila kujali maana asilia ya "maji", ilikuwa sauti tu ya "m". Waligeuza alama kulingana na mwendo wao wa kuandika kuanzia upande wa kushoto na kufikia umbo lililokaa hivyo. Waitalia wa kwanza wakaipokea ilivyo hata kama walirudia mara nyingi umbo la awali. Waroma wakaendeleza alama hiyo katika alfabeti yao kwa maana hiyohiyo.
|