Mpumalanga
Neno Mpumalanga limetokana katika lugha ya Kiswazi likimaanisha "mahali pa macheo". JiografiaMpumalanga imepakana na Eswatini na Msumbiji halafu na majimbo ya KwaZulu-Natal, Dola Huru, Gauteng na Limpopo. Hifadhi ya Kruger ambayo ni hifadhi ya wanyama mashuhuri imo jimboni. Kuna kanda mbili za tambarare za juu penye usimbishaji kidogo na tambarare za duni penye mvua nyingi. UchumiKilimoSehemu kubwa ya eneo hutumiwa kwa kilimo. Mazao ni pamoja na mahindi, ngano, ntama, alizeti, soya, karanga, miwa, mboga, kahawa, chai, pamba, tumbako, machungwa na matgunda mengine. Misitu huvunwa hasa katika kaskazini penye kiwanda kikubwa cha karatasi cha Ngodwana. Takriban 14% za eneo hutumiwa kwa mifugo hasa ng'ombe na kondoo. MigodiKati ya madini yanayochimbwa ni: dhahabu, platini, shabha, makaa mawe na mengi mengine. Mpumalanga huzalisha 83% za makaa mawe ya Afrika Kusini. UtaliiHifadhi ya Kruger ina eneo la 20,000 km² hutembelewa sana na watalii. Viungo vya nje
|