SarufiSarufi ni tawi la isimu au ni elimu ya kupanga maneno kwa ufasaha. Maelezo hayo yanaweza kutafsiriwa kwa namna mbili tofauti. Kwanza, yanaweza kutafsiriwa kwa maana ya ufunzaji wa vipashio vidogo vya lugha (sauti-silabi-neno-sentensi), kisha vipengele kama msamiati, utungaji wa sentensi kwa kutumia aina mbalimbali za maneno (nomino, vihisishi, vihusishi, vielezi, viwakilishi, [vivumishi]], vitenzi na kadhalika). Hapa kuna mambo kama methali, hadithi, vitendawili, itikadi na kadhalika. Basi huachiwa mbali. Tafsiri ya pili ya maelezo haya huchukua yote yafunzwayo katika lugha fulani. Kama maelezo ya awali, sarufi ina vipengele tofautitofauti. Ikiwa pamoja na kufunza maneno magumu, vitenzi, nyakati, matamshi, ngeli, vivumishi, nomino, vielezi na vihisishi.
|