TrilioniTrilioni (kutoka Kiingereza "trillion") ni namba ambayo inamaanisha milioni mara elfu mara elfu moja, au milioni mara milioni na kuandikwa 1,000,000,000,000. Inafuata 999,999,999,999 na kufuatwa na 1,000,000,000,001. Inaweza kuandikwa pia kifupi 1 × 1012. Matumizi tofautiHesabu ya juu inafuata Kiingereza cha Marekani; kwa lugha nyingi za Ulaya trilioni ni 1018 na 1012 wanaita "bilioni". Kimataifa kuna kawaida mbili tofauti kwa kutaja namba kuanzia milioni elfu moja au 109 [1]. Zinaitwa "skeli ndefu" na "skeli fupi":
Mifumo yote miwili hutumia silabi za namba za Kilatini bi = 2, tri = 3, quadri = 4, quinti = 5, sexti = 6 na kadhalika ila hali halisi kwa namba kubwa sana ni kawaida kutumia umbo la tarakimu lama vile 106, 109, 1012 na kadhalika. Inatokea mara nyingi ya kwamba skeli zote mbili zinachanganywa wakati wa kutafsiri vitabu au makala. Hapo ni afadhali kurudia namba kwa tarakimu. Tazama piaMarejeo
|