Share to: share facebook share twitter share wa share telegram print page

 

Umoja wa Muungano wa Afrika

Nchi za Umoja wa Maungano ya Afrika
buluu: nchi zilizounda OAU;
kijani: nchi zilizojiunga hadi 1969
kichungwa: nchi zilizojiunga hadi 1979
nyekundu:Zimbabwe ilijiunga 1982
dhambarau:nchi zilizojiunga tangu 1990

Umoja wa Muungano wa Afrika (Kiingereza: Organisation of African Unity, OAU; Kifaransa: Organisation de l'Unité Africaine, OUA) ulikuwa jumuiya ya nchi huru za Afrika iliyoanzishwa 1963 na kudumu hadi 2002. Ulikuwa mtangulizi wa Umoja wa Afrika ambao ni jumuiya ya nchi za Afrika tangu Julai 2002.

OAU iliundwa tarehe 25 Mei 1963 mjini Addis Abeba na nchi 30 za Afrika. Kwenye mkutano wa 11 Julai 2001 Mkutano Mkuu uliamua kuunda Umoja wa Afrika kama haua mpya kwenye harakati ya kuungana Afrika na OAU ilifungwa tar. 9 Julai 2002.

Mwishoni nchi zote za Afrika zilikuwa wanachama isipokuwa Moroko iliyojitenga mwaka 1985 baada ya Sahara ya Magharibi kupokelewa katika OAU.


Prefix: a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9

Portal di Ensiklopedia Dunia

Kembali kehalaman sebelumnya