Uzuri
Uzuri ni sifa ya nafsi, mnyama, mahali, tendo, wazo, neno, tungo, sauti, picha au kitu chochote kinachopendeza. Kimsingi, kwa wanaomuamini Mungu, ni sifa yake ambayo inajumlisha zile za umoja, ukweli na wema, na kujitokeza katika utakatifu wa watu wake. Kwa namna mbalimbali uzuri unachunguzwa na falsafa, sosholojia, saikolojia n.k. na kulengwa na binadamu tangu zamani za kale, hasa kwa njia ya sanaa za aina mbalimbali. Tangu mtu yupo, hawezi kuridhika na mahitaji ya mwili tu. Pengine uzuri unategemea utamaduni, lakini mara nyingi unapendeza watu wote. Mang'amuzi ya "uzuri" mara nyingi yanatokana na utambuzi wa ulinganifu na uasilia, unaomfanya mtu ajisikie salama na kuridhika. Hata hivyo, kwa kuwa mara kadhaa ni mang'amuzi ya binafsi, mithali ya Kiingereza inasema, "beauty is in the eye of the beholder" ("uzuri umo jichoni mwa mtazamaji")[1]hata pengine ni suala la urithi.[2][3] Tanbihi
Viungo vya njeWikimedia Commons ina media kuhusu:
|