Vladimir LeninVladimir Lenin
Vladimir Ilyich Lenin (kwa Kirusi: Влади́мир Ильи́ч Ле́нин; jina la kiraia: Vladimir Ilyich Ulyanov, Влади́мир Ильи́ч Улья́нов; 10 Aprili (22 Aprili ya kalenda ya Gregori) 1870 - 21 Januari 1924) alikuwa mwanasiasa nchini Urusi na kiongozi wa chama cha Bolsheviki akaendesha awamu la kikomunisti la Mapinduzi ya Urusi ya 1917 akaanzisha Umoja wa Kisovyeti. Mafundisho yake yalikuwa msingi wa itikadi ya Ulenin. Kijana katika UrusiLenin alizaliwa katika familia tajiri katika mji wa Simbirsk (sasa unaitwa Ulyanovsk). Alianza kupenda mapinduzi baada ya kaka yake kuuliwa mwaka wa 1887. Alipofukuzwa kutoka Chuo Kikuu cha Kazan kwa maandamano ya kuipinga serikali ya Tsar, alijishughulisha kupata shahada ya sheria katika miaka iliyoufuata. Alianza kutumia jina la "Lenin" kama jina la siri alipojiunga na upinzani dhidi ya serikali ya kifalme ya Kirusi. Hakuna uhakika kama alilitumia kama kumbukumbu kwa mlezi wake alipokuwa mtoto au kutokana na mto Lena katika jimbo la Siberia alipohamishwa ufungoni 1897 baada ya kushiriki katika upinzani dhidi ya serikali. Mwanamapinduzi ugeniniAlipomaliza kipindi chake cha uhamisho huko Siberia, aliondoka katika Urusi akahamia Ulaya ya Magharibi kwenye mwaka 1900. Hapa alianzisha jarida la "Iskra" alimojadili siasa ya kimapinduzi kwa Urusi. Mwaka 1903 alijiunga na Chama cha Kijamaa-Kidemokrasia cha Urusi akashiriki katika mkutano wa pili wa chama hiki kilichoanza mjini Brussels (Ubelgiji) mwisho wa Julai 1903 lakini ulipaswa kuhamishwa London baada ya siku chache kutokana na kuingilia kwa polisi ya Kibelgiji. Hapa London Lenin alipinga viongozi wengine na hapo ndipo chanzo cha "Wabolsheviki"; maana katika kura moja kundi la Lenin lilipata kura nyingi na hapo likaitwa "bolsheviki" yaani walio wengi zaidi. Wale walioungwa mkono na wachache katika kura hiyo waliitwa "mensheviki" yaani walio wachache, ingawa kwa jumla kundi la Lenin lilikuwa na wafuasi wachache katika siku zile. Mwaka 1905 Warusi waliokaa ugenini walisika habari za mapinduzi ya Urusi ya 1905. Lenin aliandika makala kuwa ni lazima kwa wanamapiduzi kuchukua silaha na kushambulia dola kwa nguvu lakini bila mafanikio ilhali Wamenshiviki katika chama walimpinga. Baada ya mapinduzi serikali ya Tsar ilipaswa kukubali kiwango kikubwa zaidi ya uhuru wa kisasa. Lenin alirudi Urusi aliposhiriki katika jarida moja mjini Sankt Petersburg akijaribu kujenga chama cha kijamaa-kidemokrasia kwa siri; ndani ya chama alipigania msimamo wa kutafuta mapinduzi kwa kutumia silaha. Alikubali pia mtindo wa kutafuta pesa kwa chama kwa njia ya ujambazi katika benki na ofisi za posta[1][2]. Mwaka 1907 Lenin alitafutwa na polisi akakimbia tena na kukaa kwanza Ufaransa, halafu Uingereza na Ujerumani. Miaka ya Vita Kuu ya KWanza ya Dunia kuanzia 1917 alikaa hasa nchini Uswisi, katika nchi ambayo haikushiriki katika vita hiyo. Leni alifauku kuimarisha nafasi yake katika chama hasa baada ya mkutano wa 1912 uliofanyika mjini Praha ambako Wabolsheviki walifaulu kushinda Wamensheviki, tukio lililosababisha kugawanyika kwa chama. Baada ya Mapinduzi ya Februari 1917 iliyompindua Tsar, huduma ya ujasusi wa Ujerumani iliwasiliana na Lenin aliyesafirishwa na Wajerumani hadi Ufini kwa sababu Wajerumani walitumaini atadhoofisha jeshi la kirusi lililoendelea kupigana na Ujerumani hata baada ya mapinduzi ya Februari[3]. Mapinduzi ya Oktoba 1917Lenin alirudi Sankt Peterburg (iliyobadilisha jina lake la Kijemrumani wakati wa vita kuwa Petrograd) kwenye Aprili 1917. Alipokelewa na umati kwenye Kituo cha Reli ya Kifini huko Petrograd. Vladimir Ilyich alitoa hotuba fupi kwa wale waliokutana naye, ambalo alitoa wito wa mapinduzi ya kijamaa. Baada ya machafuko matatu ya kisiasa ya Serikali ya Muda ya Urusi (Aprili, Juni, Julai 1917), kukandamiza uasi wa kupinga mapinduzi ya Jenerali Kornilov (Agosti 1917), ukanda mpana wa "Bolshevization" wa Soviets (Septemba 1917) , Lenin alifikia hitimisho: ukuaji wa ushawishi wa Wabolshevik na kupungua kwa mamlaka ya Serikali ya Muda kati ya watu wengi wanaofanya kazi hufanya iwezekane kwa uasi wa kuhamisha nguvu za kisiasa mikononi mwa watu. Maasi hayo yalifanyika mnamo Oktoba 25, 1917, kulingana na mtindo wa zamani. Jioni hiyo, katika mkutano wa kwanza wa Mkutano wa Pili wa Soviets, Lenin alitangaza serikali ya Soviet na amri zake mbili za kwanza: juu ya kumaliza vita na kuhamisha eneo la wamiliki wa ardhi na ardhi inayomilikiwa kibinafsi kwa matumizi yasiyolipwa ya watu wanaofanya kazi. Kwa mpango wa Lenin, mnamo 1918 Mkataba wa Brest-Litovsk ulihitimishwa na Ujerumani. Lenin aliona kwamba wakulima wa Kirusi hawataenda vitani; aliamini, zaidi ya hayo, kwamba mapinduzi ya Ujerumani yalikuwa yakiendelea kwa kasi kubwa. Baadaye kulikuwa na mapinduzi nchini Ujerumani. Lenin alisimama kwenye asili ya uundaji wa Jeshi Nyekundu, ambalo lilishinda nguvu za pamoja za mapinduzi ya ndani na nje katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kwa mapendekezo yake, Muungano wa Jamhuri za Kisoshalisti za Kisovieti uliundwa. Mwisho wa vita vya wenyewe kwa wenyewe na kukomesha uingiliaji wa kijeshi, uchumi wa kitaifa wa nchi ulianza kuimarika. Lenin alielewa hitaji la ironclad kubadilisha safu ya kisiasa ya Wabolsheviks. Kwa maana hii, kwa msisitizo wake, "Ukomunisti wa vita" ulikomeshwa, ugawaji wa chakula ulibadilishwa na ushuru wa chakula. Alianzisha kile kinachoitwa Sera Mpya ya Uchumi, ambayo iliruhusu biashara huria ya kibinafsi, ambayo ilifanya iwezekane kwa sehemu kubwa ya watu kutafuta kwa uhuru njia hizo za kujikimu ambazo serikali haikuweza kuwapa. Wakati huo huo, alisisitiza juu ya maendeleo ya makampuni ya serikali, juu ya umeme, na maendeleo ya ushirikiano. Lenin alidokeza kwamba kwa kutarajia mapinduzi ya ulimwengu ya proletarian, wakati sekta zote kubwa zikiwekwa mikononi mwa serikali, ni muhimu kujenga ujamaa polepole katika nchi moja. Yote hii inaweza kusaidia kuweka nchi ya Soviet kwenye kiwango sawa na nchi zilizoendelea zaidi za Ulaya. Lenin aliaga dunia mjini Nizhny Novgorod (Gorki karibu na Moskva) tar. 21 Januari 1924. Maiti yake ilihifadhiwa kwa madawa na kuonyeshwa katika kaburi kubwa kwenye uwanja nyekundu mjini Moskva. Kiongozi aliyemfuata alikuwa Josef Stalin. Marejeo
|