Waraka wa pili kwa WakorinthoWaraka wa pili kwa Wakorintho ni kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo. Ni kati ya barua mbili zilizomo za Mtume Paulo kwa Wakristo mjini Korintho (Ugiriki). Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu. MazingiraMdo 19:21-20:1 inasimulia Paulo alivyohama Efeso kutokana na matatizo kuzidi, akaelekea Makedonia na Ugiriki. Toka huko alipata nafasi ya kuhubiri katika Iliriko, yaani kuanzia Albania ya leo kwenda kaskazini (Rom 15:19). Wakati huo alipata habari mbaya kuhusu Wakorintho, akawaandikia tena na tena kabla hajawaendea kwa mara ya tatu. MpangilioLabda kwa kuwa ni mshono wa barua hizo mbalimbali, mpangilio wa 2Kor haueleweki, ingawa ina salamu na shukrani mwanzoni, na salamu nyingine mwishoni kama kawaida. Katikati mada kuu ni tatu: kujitetea, mchango na mashambulizi dhidi ya wapinzani. Barua hiyo inatusaidia hasa kumjua Paulo mwenyewe (2Kor 11:1-12:13). Viungo vya njeTafsiri ya Kiswahili
Vingine
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Online translations of Second Epistle to the Corinthians:
|