BarafutoBarafuto huitwa pia "mto wa barafu". Ni kanda kubwa la barafu iliyoanza kutambaa kutokana na uzito wake ikifuata graviti kwenye mtelemko. Kwa sababu hiyo barafuto zinapatikana hasa mlimani. Asili ya barafu ya barafutoBarafuto zimetokana na theluji inayokaa miaka mingi bila kuyeyuka katika mazingira baridi. Theluji mpya inakaa juu ya theluji ya miaka iliyotangulia. Uzito wa theluji ya baadaye inakandamiza ile ya chini. Kutokana na shindikizo hili theluji ya chini hubadilika kuwa barafu kabisa. Barafuto ni kati ya nguvu kubwa za mmomonyoko duniani. Afrika ina barafuto ndogo kadhaa juu ya mlima Kilimanjaro na mlima Kenya lakini zinaelekea kupotea kutokana na uhaba wa mvua itakayobadilika kuwa theluji mpya. Zamani za enzi ya barafu kiwango cha barafu kwenye ncha ya kaskazini kilikuwa kikubwa kiasi cha kusababisha barafuto kutokea zilizosukuma barafu hadi Ulaya ya Kati.
|