Muungano wa Madola ya Amerika (kwa Kiingereza: United States of America), hujulikana pia kama Marekani (kwa Kiingereza: United States, US, USA au America), ni nchi inayopakana na Kanada na Meksiko katika Amerika ya Kaskazini, mbali ya kuundwa pia na visiwa vya Hawaii.
Eneo la Marekani lina ukubwa wa kilometa mraba 9,826,675 na liko hasa katika bara la Amerika Kaskazini kati ya Kanada upande wa kaskazini na Meksiko upande wa kusini.
Marekani imeunganisha upana wote wa bara kutoka Bahari ya Atlantiki hadi Pasifiki, ikigawanywa kwa majimbo 48 yanayojitawala.
Jimbo la Alaska liko pia kwenye bara la Amerika Kaskazini upande wa kaskazini kutoka Kanada kuelekea Urusi, lakini halipakani na jimbo lolote la Marekani.
Hawaii
Funguvisiwa la Hawaii ni jimbo la visiwani katika bahari ya Pasifiki. Ni jimbo la 50 na la mwisho mpaka sasa.
Visiwa vya ng'ambo vya Marekani
Maeneo ya ng'ambo ya Marekani ni visiwa kadhaa ambavyo ni maeneo ya Kimarekani ingawa si sehemu ya jimbo lolote. Zamani yalikuwa kama makoloni hata kama Marekani ilidai kutokuwa na ukoloni. Siku hizi maeneo haya yamepata viwango mbalimbali vya kujitawala. Kwa kawaida maeneo haya huchagua pia wawakilishi kwa ajili ya bunge la Marekani lakini wawakilishi hao si wabunge wa kawaida, bali wana haki ya kusema na kushauri tu bila haki ya kupiga kura.
Kwa namna hiyo, mazingira ya Amerika yalibadilika kabisa mpaka zikatokea aina mpya za utamaduni na hatimaye mataifa mapya, hasa kutokana na mchanganyiko ya wenyeji (Waindio) na walowezi kutoka Ulaya, halafu pia watumwa kutoka Afrika.
Katika vita dhidi ya Hispania na Meksiko, Marekani ilipanua eneo lake kwenda kusini.
Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani ilipigwa kuanzia 1861 hadi 1865 kati ya majimbo ya kusini na majimbo ya kaskazini nchini Marekani. Sababu mojawapo muhimu ya vita ilikuwa suala la utumwa. Majimbo ya kaskazini yaliwahi kupiga utumwa marufuku lakini majimbo ya kusini yaliendelea na sheria zilizoruhusu utumwa na matajiri wengi wa kusini walitegemea kazi ya watumwa hao. Mafarakano yalianza kuhusu swali kama madola mapya yaliyoanzishwa katika Amerika Kaskazini na kujiunga na Muungano yangeruhusiwa kukubali utumwa au la. Mwaka 1861 madola ya kusini-mashariki yalitangaza kujiondoa katika Muungano na kuanzisha "Shirikisho la Madola ya Amerika". Vita vilianza na kudumu miaka minne na watu 650.000 walikufa, lakini mwishoni kaskazini ilishinda. Utumwa ulipigwa marufuku na watumwa walipewa haki za kiraia. Lakini watumwa wengi wa awali waliendelea kuwa maskini na baada ya muda, sheria mpya katika majimbo ya kusini zilinyima haki nyingi za kiraia za Wamarekani weusi waliopaswa kuishi chini mfumo wa ubaguzi wa rangi.
Katika miongo iliyofuata, Marekani ilitwaa maeneo yaliyowahi kubaki chini ya mamlaka ya Waindio na kuyafanya maeneo yake. Katika Vita vya Marekani dhidi ya Hispania kwenye mwaka 1898 ilijipatia utawala juu ya Ufilipino na Puerto Rico, makoloni ya awali ya Hispania, na kuwa yenyewe nchi iliyotawala makoloni.
Katika siasa ya nje, Marekani iliwahi kutangaza tangu mwaka 1823 kwamba ilitazama Amerika yote kama eneo ambalo haikubali kuingiliwa na nchi za Ulaya; wakati ule makoloni mengi ya Amerika ya Kusini yalikuwa yakifaulu kupata uhuru kutoka Hispania, na Marekani ilitaka kusisitiza isingekubali kuingia kwa mataifa mengine ya Ulaya.
Katika miongo iliyofuata uchumi wa Marekani uliimarika pamoja na kukua kwa sekta ya viwanda na wafanyabiashara wa Marekani walipanua biashara yao kimataifa; mnamo 1854manowari za Marekani ziliilazimisha Japani kukubali kufunguliwa kwa ubalozi na kupokea wafanyabiashara. Meli za wafanyabiashara wa Marekani zilifika kote duniani, tangu miaka ya 1830 hadi Zanzibar ambako ubalozi mdogo ulifunguliwa mwaka 1837[2]. Wakati wa vita dhidi ya Hispania Marekani ilihakikisha pia nafasi yake katika biashara ya China dhidi ya mipango ya mataifa ya Ulaya ya kuigawa nchi hiyo.
Katika miongo ya vita baridi iliyofuata, Marekani ilikuwa taifa la kuongoza nchi zenye demokrasia na pia zile ambazo zilisimama upande wa ubepari tu bila demokrasia dhidi ya nchi za kikomunisti zilizoongozwa na Umoja wa Kisovyeti.
Vilevile miaka ya 1960 ilikuwa kipindi cha mapambano kwa ajili ya haki za Wamarekani weusi, wajukuu wa watumwa wa awali hasa kusini mwa Marekani. Sheria zilizotenganisha watu pamoja na matumizi ya shule, vyuo, majengo na taasisi za burudani kulingana na rangi ya ngozi, zilizozuia ndoa kati ya watu wa rangi tofauti na kuzuia watu maskini wasitumie haki za kiraia zilipigwa marufuku bila kuondoa tofauti katika uwezo wa kiuchumi kati ya makundi katika jamii.
Nchi ina wakazi zaidi ya milioni 333, na ina mchanganyiko mkubwa wa asili kuliko nyingine yoyote duniani. Waliojitambulisha kama Wazungu ni 61.6%, Waafrika 12.6%, Waasia 6%, Waindio 1.1%, machotara 10.2% n.k.
Wakazi wengine wanatumia lugha nyingine nyingi, hasa kulingana na nchi ya asili ya ukoo wao. Kati ya lugha hizo, inaongoza kwa mbali ile ya Kihispania (milioni 37). Nyingine ni Kichina, Kitagalog, Kivietnam, Kifaransa, Kikorea na Kijerumani.
Dini
Nchini dini zote zina uhuru mkubwa, tena kwa asilimia 59 ya wakazi dini ina umuhimu wa hali ya juu, tofauti na nchi tajiri nyingine duniani.
↑Gilbert, Wesley. Our Man in Zanzibar: Richard Waters, American Consul (1837-1845), tasnifu 2011 kwenye Wesleyan University, Middletown, Connecticut online hapa
Viungo vya Nje
Acharya, Viral V.; Cooley, Thomas F.; Richardson, Matthew P.; Walter, Ingo (2010). Regulating Wall Street: The Dodd-Frank Act and the New Architecture of Global Finance. Wiley. uk. 592. ISBN978-0-470-76877-8.
Barth, James; Jahera, John (2010). "US Enacts Sweeping Financial Reform Legislation". Journal of Financial Economic Policy. 2 (3): 192–195.
Berkin, Carol; Miller, Christopher L.; Cherny, Robert W.; Gormly, James L. (2007). Making America: A History of the United States, Volume I: To 1877. Cengage Learning. uk. 75., Book
Boyer, Paul S.; Clark, Clifford E. Jr.; Kett, Joseph F.; Salisbury, Neal; Sitkoff, Harvard; Woloch, Nancy (2007). The Enduring Vision: A History of the American People. Cengage Learning. uk. 588. ISBN978-0-618-80161-9., Book
Clingan, Edmund. An Introduction to Modern Western Civilization. iUniverse. ISBN978-1-4620-5439-8., Book
Calloway, Colin G. New Worlds for All: Indians, Europeans, and the Remaking of Early America. JHU Press. uk. 229. ISBN978-0-8018-5959-5., Book
Ferguson, Thomas; Rogers, Joel (1986). "The Myth of America's Turn to the Right". The Atlantic. 257 (5): 43–53. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-01-04. Iliwekwa mnamo Machi 11, 2013. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Lemon, James T. (1987). "Colonial America in the 18th Century". Katika Robert D. Mitchell; Paul A. Groves (whr.). North America: the historical geography of a changing continent. Rowman & Littlefield., PDFIlihifadhiwa 23 Januari 2013 kwenye Wayback Machine.
Smith, Andrew F. (2004). The Oxford Encyclopedia of Food and Drink in America. New York: Oxford University Press, pp. 131–32. ISBN 0-19-515437-1.
Soss, Joe (2010). Hacker, Jacob S.; Mettler, Suzanne (whr.). Remaking America: Democracy and Public Policy in an Age of Inequality. Russell Sage Foundation. ISBN978-1-61044-694-5., Book
Tadman, Michael (2000). The Demographic Cost of Sugar: Debates on Slave Societies and Natural Increase in the Americas. Juz. la 105. Oxford University Press. {{cite book}}: |journal= ignored (help), Article
Taylor, Alan (2002). Eric Foner (mhr.). American Colonies: The Settling of North America. Penguin Books, New York. ISBN0-670-87282-2., Book
Vaughan, Alden T. (1999). New England Encounters: Indians and Euroamericans Ca. 1600–1850. North Eastern University Press.
Walton, Gary M.; Rockoff, Hugh (2009). History of the American Economy. Cengage Learning., Book
Williams, Daniel K. (2012). "Questioning Conservatism's Ascendancy: A Reexamination of the Rightward Shift in Modern American Politics; {Reviews in American History}". 40 (2). The Johns Hopkins University Press: 325–331. {{cite journal}}: Cite journal requires |journal= (help)
Cohen, Eliot A. (Julai–Agosti 2004). "History and the Hyperpower". Foreign Affairs. Washington D.C. Iliwekwa mnamo Julai 14, 2006.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Marekani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.