Saint Lucia
Saint Lucia ni nchi ya kisiwani katika bahari ya Karibi na sehemu ya visiwa vya Antili Ndogo. Iko katikati ya visiwa vya Saint Vincent na Grenadini, Barbados na Martinique. Kisiwa kina asili ya volkeno na eneo la milimamilima. Jina linatokana na lile la Mtakatifu Lusia na kulifanya nchi pekee duniani yenye jina la mwanamke. WatuWakazi walio wengi ni wa asili ya Afrika (85.3%), halafu machotara Waafrika-Wazungu na Waafrika-Wahindi (10.9%), Wahindi (2.2%), Wazungu (0.6%). Lugha rasmi ni Kiingereza, lakini wananchi wengi (95%) wanaongea kwa kawaida Patwah, Krioli inayotokana na Kifaransa na kufanana na Kihaiti. Upande wa dini, wengi ni Wakristo: 62.5% ni Wakatoliki, 24.5% ni Waprotestanti (7% Waadventista Wasabato, 6% Wapentekoste, n.k.), 1.9% ni Warastafari, 1.4% Wahindu n.k. Tazama piaViungo vya nje
|