Belize
Inapakana na nchi za Mexiko, Guatemala na Honduras. Makao makuu yako Belmopan, lakini mji mkubwa zaidi ni Belize. HistoriaHadi mwaka 1973 ilijulikana kama koloni la British Honduras (Honduras ya Kiingereza). Tangu mwaka 1964 koloni lilikuwa na serikali yake na madaraka ya kujitawala katika mambo ya ndani. Uhuru kamili ukafuata tarehe 21 Septemba 1981. Uhusiano na nchi jirani ya Guatemala ulikuwa mgumu kwa miaka mingi kwa sababu serikali ya Guatemala ilidai kuwa Belize ni sehemu yake. WatuIngawa wakazi si wengi, wana asili tofauti sana. Walio wengi ni machotara: kati yao, 52.9% wana damu ya Waindio zaidi, 32% damu ya Kiafrika zaidi. Wanafuata kwa wingi Waindio asili, Wahindi, Wazungu, Wachina n.k. Lugha rasmi ni Kiingereza, lakini kwa kawaida zinazungumzwa Krioli (62.6%) na Kihispania (30%). Upande wa dini, 73.8% ni Wakristo (40.1% ni Wakatoliki na 31.8% Waprotestanti wa madhehebu mbalimbali). 15.5% hawana dini yoyote. Tazama pia
|