Georgia ni jimbo lililopo Kusini-Mashariki mwa Marekani.Linapakana kaskazini na Tennessee pamoja na Carolina Kaskazini, huku upande wa mashariki ikipakana na Carolina Kusini na Bahari ya Atlantiki. Florida iko upande wa kusini, na Alabama iko magharibi. Kwa ukubwa wa eneo, Georgia inashika nafasi ya 24 kati ya majimbo ya Marekani, na kwa idadi ya watu, ni ya nane. Idadi ya watu wa Georgia inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 11 kufikia mwaka 2024. Atlanta ni mji mkuu wa jimbo na pia kitovu kikuu chenye idadi kubwa ya watu. Ukanda wa jiji la Atlanta una zaidi ya watu milioni 6 na unajumuisha zaidi ya nusu ya wakazi wote wa jimbo. Miji mingine mashuhuri ni Augusta, Savannah, Columbus, na Macon.
Georgia ilikuwa kati ya koloni asilia 13 za Kiingereza katika Amerika ya Kaskazini zilizoasi dhidi ya Uingereza 1776 ikawa jimbo la Marekani 1788.
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Georgia (jimbo) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.