Montana
Montana ni jimbo la kujitawala la Maungano ya Madola ya Amerika au Marekani. Iko katika kaskazini ya nchi mpakani na Kanada ikipakana na majimbo ya North Dakota, South Dakota, Wyoming na Idaho. Mji mkuu ni Helena na mji mkubwa jimboni ni Billings. Jimbo lina wakazi 944,632 pekee wanaokalia eneo la kilomita za mraba 380,700 (ambayo ni kubwa kuliko Kenya). Takriban asilimia 6,3 % za wakazi ni Waindio au wenyeji asilia. Jimbo lina milima mingi. Montana ni hasa jimbo la kilimo cha mahindi na ngano pamoja na ufugaji wa ng'ombe. Kuna maliasili nyingi pia kama vile shaba, dhahabu, almasi, antimoni, fosfeti, mafuta ya petroli, gesi na makaa mawe. Eneo la Montana lilitwaliwa na Marekani tangu miaka ya 1850 na 1889 eneo likapewa cheo cha jimbo kamili. Wikimedia Commons ina media kuhusu:
|