Share to: share facebook share twitter share wa share telegram print page

 

Kateri Tekakwitha

Picha yake ya zamani kuliko zote, mwaka 1690 hivi.

Kateri Tekakwitha (kwa lugha yake ya Kimohawk jina linatamkwa ˈgaderi degaˈgwita) aliishi tangu mwaka 1656 hadi 17 Aprili 1680; alizaliwa Ossernenon, leo Auriesville, New York, Marekani, akafariki Kahnawake, Quebec Canada[1].

Mtoto wa familia ya wakazi asili wa Amerika Kaskazini, anajulikana hasa kwa imani na maadili yake ya Kikristo, dini aliyojiunga nayo kwa kubatizwa na padri wa Kanisa Katoliki[2][3] kwenye Pasaka ya mwaka 1676, akaendelea nayo bila kujali vitisho na upinzani wa ndugu zake, akishika pia usafi wa moyo aliokuwa amenuia kuutunza tangu kabla ya kuwa Mkristo.

Alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri tarehe 22 Juni 1980, halafu Papa Benedikto XVI akamtangaza mtakatifu tarehe 21 Oktoba 2012. Ni wa kwanza kutoka makabila ya Waindio.

Anaheshimiwa kama mtakatifu bikira, hasa tarehe ya kifo chake[4].

Tazama pia

Tanbihi

  1. Pierre Cholence, S.J., "Catharinae Tekakwitha, Virginis" (1696), Acta Apostolica Sedis, 30 Januari 1961
  2. Pierre Cholenec, S.J. (1696). The Life of Catherine Tekakwitha, First Iroquois Virgin. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-25. Iliwekwa mnamo 2012-02-18.
  3. Claude Chauchetiere, S.J. (1695). "The Life of the Good Catherine Tekakwitha, said now Saint Catherine Tekakwitha". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-25. Iliwekwa mnamo 2012-02-18.
  4. Martyrologium Romanum

Marejeo

  • Bechard, Henri. "Tekakwitha". Dictionary of Canadian Biography (Toronto: University of Toronto Press, 1966), vol. 1.
  • Sargent, Daniel. Catherine Tekakwitha. New York and Toronto: Longmans, Green and Co., 1936.
  • Shoemaker, Nancy. "Kateri Tekakwitha's Tortuous Path to Sainthood," in Nancy Shoemaker, ed. Negotiators of Change: Historical Perspectives on Native American Women (New York: Routledge, 1995), p. 49–71.
  • Steckley, John. Beyond their Years: Five Native Women's Stories, Canadian Scholars Press 1999 ISBN 978-1551301501

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
Prefix: a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9

Portal di Ensiklopedia Dunia

Kembali kehalaman sebelumnya