Barbara KimBarbara Kim (1805 - Seoul, 27 Mei 1839) alikuwa mjane aliyefariki kwa tauni gerezani alipokuwa amefungwa kwa sababu ya imani yake ya Kikristo. Ni mmojawapo katika kundi kubwa la waumini wa Kanisa Katoliki nchini Korea waliouawa katika miaka 1791–1888. Wanakadiriwa kuwa 8,000 - 10,000. Yeye na wenzake 102 walitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984.[1] Sikukuu ya hao Wafiadini wa Korea huadhimishwa tarehe 20 Septemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 27 Mei[2]. MazingiraMwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu nchini[3] kwa juhudi za wananchi walei. Mwaka 1836 Korea, nchi ya Kikonfusyo ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society)[4]. Chini ya nasaba ya Joseon, Ukristo ulifutwa, tena waamini walidhulumiwa na kuuawa. Waliobaki walipaswa kushika imani yao kwa siri. Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
|