Inaweza kufanywa na mtu binafsi au na kundi, hasa likiongozwa na kuhani au mwingine aliyekubalika.
Dini zinaelekeza binadamu kufanya ibada inavyotakiwa.
Ibada inasisitiza ukweli wa yule anayetolewa heshima hiyo, kwa mfano kutokana na imani ya dini fulani.[1] Vilevile ukweli wa mtoaji kwa maana ibada lazima itoke moyoni: ndiyo sababu haiwezi kulazimishwa.
↑Kuhusu swalah tano, Mtume aliripotiwa kusema, Swalini kama munavoniona mimi nikiswali [Imepokewa na Bukhari]
Aisha alipokewa kwamba alisema: (Mtume alikuwa akifungua Swalah kwa Takbiri na kisomo cha “Alhamdu lillaahi Rabbil ‘aalamiin”, na alikuwa akirukuu hakiinamisha kichwa chake na wala hakisimamishi sawa, bali alikiweka baina ya hali hizo mbili. Na alikuwa akiinua kichwa chake kutoka kwenye rukuu, hasujudu mpaka alingane katika kusimama. Na alikuwa akisoma Atahiyatu katika kila rakaa mbili, na alikuwa akikalia mguu wake wa kushoto na akiusimamisha mguu wake wa kulia. Na alikuwa akikataza mkao wa Shetani (kukaa kama shetani) na alikikataza mtu kuiweka chini mikono yake katika kukaa kama vile mnyama wa kuwinda, na alikuwa akihitimisha Swala yake kwa kupiga Salamu) [Imepokewa na Muslim.]
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.