JangwaJangwa ni eneo kavu lenye mvua au usimbishaji kidogo tu. Kutokana na ukavu kuna mimea michache tu, pia wanyama wachache. Wanyama walioko hufanya shughuli zao hasa wakati wa usiku. Kipimo cha usimbishaji kinachotambulika kimataifa ni kiwango cha chini ya mm 250 kwa mwaka[1]. Uoto wa mimea hufunika chini ya asilimia 5 za eneo lake. Wakati mwingine huitwa jangwa hata maeneo ambayo ni makavu kutokana na baridi kali. Aina za maeneo makavu: jangwa na mibugaMaeneo makavu yanaweza kutofautishwa kuwa yabisi sana (en: extremely arid) pasipo usimbishaji kwa muda wa miezi 12 mfululizo (maana yake hakuna mvua kila mwaka), yabisi (en: arid) pasipo usimbishaji zaidi ya mm 250 kwa mwaka, nusu yabisi (en:semiarid) penye usimbishaji kati ya mm 250 and 500 kwa mwaka. Maeneo yabisi sana na maeneo yabisi ni jangwa. Maeneo nusu yabisi yenye nyasi huitwa mbuga. Takriban theluthi moja ya uso wa nchi kavu duniani ni yabisi sana, yabisi au nusu yabisi. Athari ya uvukizajiKiasi cha usimbishaji peke yake hakitoshi kila mahali kutofautisha maeneo makavu. Mm 200 za mvua katika eneo la joto zitasababisha eneo kuonekana kama jangwa kabisa kwa sababu kiasi kikubwa cha maji yale kidogo yanayoneshewa hupotea kutokana na uvukizaji. Kuna mifano ya kwamba eneo penye kiasi kilekile cha 200 mm halionekani kuwa jangwa tayari kwa sababu kutokana na halijoto na mawingu (hata yasiponyesha mvua) kiasi kidogo cha maji yanavukiza. Kama uvukizaji unapita kiasi cha mvua hata eneo penye mvua zaidi ya 250 mm inaonekana kama jangwa. Aina za jangwaMara nyingi majangwa hutofautishwa kutokana na uso wake:
MajiJangwa ni eneo kavu lakini maji hutokea. Maji ya chiniMara nyingi kuna maji chini ya ardhi. Pale ambako maji haya si chini mno mimea inaweza kuyafikia kwa mizizi yao. Mahali kadhaa chemchemi hutokea. Sehemu kama hizi zinaonekana kama oasisi penye miti, wakati mwingine hata na bwawa. Mahali pengine wakazi wa jangwa wamechimba kisima kirefu pasipo na mimea kinachosaidia maji ya watu na wanyama hasa wa misafara. Maji ya mvuaMvua ikionyesha unaweza kutokea kwa wingi. Maji yake hukusanyika katika mabonde na kutokea kama mto wa muda. Kuna mifano mingi ya wasafiri jangwani waliokufa kwa sababu walipiga kambi katika bonde penye kivuli lakini walizama kwa sababu mto mkali ulijitokeza kwa ghafla kutokana na mvua ulionyesha katika umbali mkubwa. Sehemu nyingine mvua husababisha kutokea kwa mbwawa hata maziwa kwa muda. Mito inayopita jangwaMito kadhaa kama Nile ina maji ya kutosha ili ivuke neo la jangwa. Inawezesha maisha ya mimea, wanyama na watu katika mabonde yao. Mito mingine inakwisha jangwani kwa sababu maji yote hupotea na kuvukiza. Mfano wake ni delta ya mto wa Okavango unaokwisha katika jangwa la Kalahari huko Botswana. Delta hii ni eneo la mimea na wanyama wengi katikati ya jangwa. Mto wa Ewaso Nyiro katika Kenya ya kaskazini kwa kawaida hukwisha katika nchi yabisi za Usamburu. Lakini kila baada ya miaka makumi kadhaa baada ya mvua kubwa sana inaendelea kuvuka jangwa la Somalia ya kusini na kufikia Bahari Hindi jinsi ilvyotokea wakati wa El-Nino 1998.
Majangwa makubwa duniani
Marejeo
|