Mnara wa BabeliMnara wa Babeli ni jengo kubwa linalotajwa katika Biblia kwenye Kitabu cha Mwanzo 11:1-9. Kufuatana na taarifa hii mnara ulijengwa pamoja na mji wa Babeli kama kilele chake. Katika mapokeo ya Mwanzo 11 Babeli ulikuwa mji wa kwanza uliojengwa baada ya gharika kuu. Binadamu waliamua kuwa na jengo kubwa katika mji na kilele chake kifike mbinguni. Mpango huu haukumpendeza Mungu aliyechanganya lugha ya watu ambao hivyo walilazimika kuachana baadaye bila ya kukamilisha mnara wao. Kihistoria si wazi ni kipindi gani kinachoangaliwa katika simulizi la Mwanzo 11. Inaonekana ya kwamba wasimulizi walikuwa na habari za piramidi au zigurati kubwa zilizokuwepo Babeli na penginepo katika Mesopotamia. Maelezo ya kiimaniSimulizi limechukuliwa kwa njia mbalimbali katika mapokeo ya Wayahudi na Wakristo. Moja ni kwamba hadithi hiyo inafundisha kwamba kiburi na dhambi kwa jumla vinatenganisha watu wasiweze kuelewana wala kuishi pamoja. Isipokuwa si wazi dhambi ni ipi. Kwa Wakristo Mwinjili Luka katika kitabu cha Matendo ya Mitume kwenye Agano Jipya alitumia mfano wa mnara kama kinyume cha matokeo ya siku ya Pentekoste ambako watu kutoka lugha mbalimbali walipata kuelewana kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Simulizi la Mwanzo 11, 1-911,1 Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja. Viungo vya njeWikimedia Commons ina media kuhusu:
Information related to Mnara wa Babeli |