Nyuzilandi
Nyuzilandi (kwa Kiingereza: New Zealand; kwa Kimaori: Aotearoa) ni nchi ya visiwani katika Pasifiki takriban km 1,500 upande wa mashariki-kusini wa Australia. Inajumuisha maeneo mawili makuu ya ardhi—Kisiwa cha Kaskazini (Te Ika-a-Māui) na Kisiwa cha Kusini (Te Waipounamu). Ni nchi ya visiwa ya sita kwa ukubwa kwa eneo na iko mashariki ya Australia kupitia Bahari ya Tasmania na kusini mwa visiwa vya New Caledonia, Fiji, na Tonga. Eneo lake linaundwa na visiwa viwili vikubwa: Kisiwa cha Kaskazini (North Island au Te Ika-a-Māui) na Kisiwa cha Kusini (South Island au Te Waipounamu) na vingine 600 vidogo. JiografiaMiji
Miji mingine ni:
WatuIdadi ya wakazi ni 4,690,000. Wengi wao (74%) bado wana asili ya Ulaya, ingawa asilimia yao inazidi kupungua. Wakazi asilia ni Wamaori waliotokea Polinesia na kuhamia visiwa hivyo kati ya miaka 1250-1300 BK; kwa sasa ni 14.9% ya wakazi wote. Wengine wana asili ya Asia (11.8%) na ya visiwa vya Pasifiki (7.4%). Lugha rasmi ni Kiingereza, Kimaori na Lugha ya Ishara ya Nyuzilandi (kwa Kiingereza: New Zealand Sign Language au NZSL). Upande wa dini, 49% ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali, kuanzia Kanisa Katoliki (12.6%), Anglikana (11.8%) na Wapresbiteri (8.5%). Idadi ya wasio na dini inazidi kupanda na imeshafikia 38.55%, mbali ya 12.27% wasiojibu swali kuhusu hilo. Kuna Mabanyani (2.1%), Wabuddha (1.5%), Waislamu (1.2%), Singasinga (0.5%) Tazama piaViungo vya nje
Information related to Nyuzilandi |