Yeroboamu IIYeroboamu II (kwa Kiebrania ירבעם השני au יָרָבְעָם; kwa Kigiriki Ιεροβοάμ; kwa Kilatini Jeroboam) alikuwa mwana na mwandamizi wa Yehoashi wa Israeli kama mtawala wa 14 wa Ufalme wa Israeli, ambao aliuongoza kwa mafanikio makubwa miaka 41. Hata hivyo Biblia haisisitizi mafanikio hayo, bali inamhukumu kwa kufuata sera ya kidini ya Yeroboamu I iliyowataka Waisraeli wamuabudu YHWH kwa sura ya fahali ya dhahabu katika mahekalu ya Dani na Beteli ili wasiende Yerusalemu, mji mkuu wa ufalme wa ukoo wa Daudi HistoriaWilliam F. Albright alikadiria ufalme wake kudumu tangu mwaka 786 KK – hadi 746 KK, wakati E. R. Thiele alisema kuwa alitawala pamoja na baba yake tangu 793 KK hadi 782 KK, halafu peke yake hadi mwaka 753 KK.[1] Alishinda Syria (2Fal 14:26, 27), aliteka Damasko (14:28), na kurudisha mipaka ya Israel ilivyokuwa wakati wa mfalme Daudi.[2] Katika BibliaAgano la Kale linamtaja tu katika Kitabu cha Pili cha Wafalme 13:13; 14:16, 23, 27, 28, 29; 15:1, 8; Kitabu cha Kwanza cha Mambo ya Nyakati 5:17; Hosea 1:1; na Amosi 1:1; 7:9, 10, 11. Tanbihi
Viungo vya nje
|