AngahewaAngahewa ni matabaka ya gesi za hewa yanayozingira sayari au gimba lingine la angani yakishikwa na uvutano wa gimba husika. Angahewa ya DuniaAngahewa inakinga uhai duniani kwa kupunguza mnururisho wa urujuanimno wa Jua, kutunza halijoto duniani kwa kuakisisha mawimbi ya mialekundu, kupunguza tofauti kati ya baridi na joto na kuwapa wanyama na mimea viwango vya oksijeni na nitrojeni wanavyohitaji. Magimba ya angani mengine kama sayari au Jua huwa pia na aina za angahewa ingawa gesi zake ni tofauti na za duniani. Gesi zilizopo katika angahewa ya Dunia ni hasa nitrojeni (78%) na oksijeni (21%) pamoja na viwango vidogo lakini muhimu vya arigoni (0.9%), dioksidi kabonia (0.035%), mvuke wa maji na gesi nyingine mbalimbali. Angahewa haina mwisho kamili, ila inazidi kuwa hafifu jinsi inavyofikia juu. Asilimia 75 za masi ya hewa yake iko katika angavungu hadi kilomita 11 juu ya uso wa Dunia. Uzito wa hewa hupimwa kama kanieneo angahewa. Halijoto na matabaka ya angahewaSehemu za angahewa zina baridi au joto zaidi kutegemeana na kimo. Tukipaa juu ya uso wa Dunia halijoto inazidi kuwa baridi, baadaye joto tena, kadiri jinsi tunavyopaa. Mabadiliko ya halijoto yanafuata muundo wa tabaka zinazotofautishwa na kiwango cha joto au baridi kinachopimwa. Kwa jumla inawezekana kutofautisha matabaka 5 ambayo ni
Matabaka ya juu, yaani tabakajoto na tabakanje, huitwa pia angaioni kwa sababu atomu za gesi zake zinapatikana katika hali ya ioni zilizopoteza elektroni kutokana na kupigwa na miale ya Jua iliyo bado kali sana hapo nje. Angahewa kwenye sayariNje ya Dunia yetu angahewa imetambuliwa pia kwenye sayari nyingine. Katika Mfumo wa Jua kuna sayari 4 za ndani zinazofanana kiasi, ni Utaridi, Zuhura, Dunia na Mirihi. Zote nne ni sayari zinazofanywa na mwamba.
Sayari kubwa za nje kama Mshtarii na Zohari si rahisi vile kuofautisha kati ya sayari yenyewe na angahewa yake. Sayari hizi huitwa pia "jitu za gesi" kwa sababu asilimia kubwa ya sayari yote ni elementi kama hidrojeni na heli ambazo kwetu duniani zinapatikana kama gesi. Kutokana na umbali mkubwa na Jua ni baridi zaidi hadi gesi hizi kupitia katika hali mango. Vilevile hidrojeni katika kiini cha Mshtarii inaaminiwa kuwa katika hali metalia kutokana na shinikizo kubwa ya masi yake. Kuna miezi kadhaa zinazunguka sayari za Jua ambako angahewa zimegundliwa, kwa mfano kwa mwezi Titani wa Zohali na miezi ya Europa na Ganimedi ya Mshtarii. Viungo vya Nje |