Bahari ya OkhotskBahari ya Okhotsk ni bahari ya pembeni ya Pasifiki ya magharibi. [1] Iko kati ya rasi ya Kamchatka upande wa mashariki, visiwa vya Kurili upande wa kusini mashariki, kisiwa cha Hokkaidō upande wa kusini, kisiwa cha Sakhalin kwenye magharibi, na pwani ya Siberia ya mashariki upande wa magharibi na kaskazini. Ghuba ya Shelikhov iko upande wa kaskazini mashariki. Jina limetokana na mji wa Okhotsk ambayo ni mji wa kwanza ulioundwa na Warusi katika Mashariki ya Mbali. JiografiaEneo la Bahari ya Okhotsk ni km2 1,583,000. Imeunganishwa na Bahari ya Japani upande wa magharibi kupitia Ghuba ya Sakhalin, upande wa kusini kupitia mlangobahari wa La Pérouse. Kina cha wastani ni mita 859, kina kirefu zaidi ni mita 3,372. Katika majira ya baridi, usafiri kwenye Bahari ya Okhotsk unakuwa mgumu, au hata hauwezekani, kwa sababu ya wingi wa barafu. VisiwaBaadhi ya visiwa vya Bahari ya Okhotsk ni vikubwa kiasi. Hii ni pamoja na Hokkaido ambayo ni kisiwa cha pili kwa ukubwa cha Japani, na Sakhalin ambayo ni kisiwa kikubwa cha Urusi. Visiwa vingi vidogo vya bahari hiyo havina wakazi, hivyo ni maeneo bora ya kuzaliana kwa sili na pinnipedia wa spishi mbalimbali pamoja na ndege wa baharini. Bandari za maana
Marejeo
Tovuti za NjeWikimedia Commons ina media kuhusu:
|