Ghuba ya UthaiGhuba ya Uthai (kwa Kiingereza: Gulf of Thailand) ni mkono wa Bahari ya China Kusini. [1] JiografiaGhuba ya Uthai imepakana na nchi za Kambodia, Uthail na Vietnam. Ncha ya kaskazini ya ghuba hiyo ni Hori ya Bangkok kwenye mdomo wa Mto Chao Phraya. Eneo la maji ni karibu km² 320,000. Mpaka wa ghuba hufafanuliwa na mstari kutoka Rasi Bai Bung kusini mwa Vietnam hadi mji wa Kota Baru kwenye pwani ya Malaysia. Ghuba ya Uthai haina kina kirefu. Kina cha wastani ni mita 45, na kina cha juu ni mita 80 tu. Inapokea maji mengi kutoka mito na hivyo uchumvi wa ghuba ni dhaifu (3.05-3.25 % pekee). Mito mikuu inayoingia ni Chao Phraya, Mto Mae Klong na Mto Bang Pakong kwenye Hori ya Bangkok, halafu Mto Tapi unaoishia katika Hori ya Bandon kusini magharibi mwa ghuba. UtaliiGhuba ya Thailand ina miamba tumbawe mingi, na vituo vya watalii vya kupiga mbizi. Watalii wanapenda sehemu hii kwa sababu hakuna baridi. Kuna sehemu nyingi zinazotembelewa na watalii katika Ghuba ya Uthai zikiwa pamoja na visiwa vya Ko Samui na Ko Pha Ngan, Pattaya, Cha-am, Hua Hin, Ko Samet na Ko Chang. Marejeo
Tovuti za NjeWikimedia Commons ina media kuhusu:
|