Bahari ya Kusini ya ChinaBahari ya Kusini ya China ni bahari ya kando ya Pasifiki mbele ya pwani la kusini ya China. Imepanuka kati ya Taiwan upande wa kaskazini na Singapur upande wa kusini. Upande wa mashariki hupakanwa na visiwa vya Indonesia na Ufilipino, upande wa magharibi na Asia bara. Nchi zinazopakana na Bahari ya Kusini ya China ni: China, Macau, Hong Kong, Taiwan, Ufilipino, Malaysia, Brunei, Indonesia, Singapur, Uthai, Kambodia na Vietnam. Mito mikubwa inayomwaga maji yao baharini ni pamoja na Mto Lulu, Min, Jiulong, Mto Mwekundu, Mekong, Pahang na Pasig. Kati ya nchi jirani kuna uvutano kuhusu mipaka na hasa haki juu ya visiwa vidogo vya Spratley na Paracelsus visivyo na wakazi lakini vina dalili za kuwa na maliasili kama mafuta ya petroli. Visiwa hivyi vyote vina pia umuhimu wa kijeshi na kisaisa kwa sababu njia za maji zinazotumiwa zaidi dunaini zinapita humo. Kila ugomvi au vita inaweza kuhatarisha mawasilano na uchumi wa nchi zinazotegemea usafiri huu.
|