Bonde la Songwe
Bonde la Songwe ni kata ya Wilaya ya Mbeya Vijijini katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania. Kata hili liko kwenye bonde la mto Songwe ya Kaskazini unapokutana nana barabara ya TANZAM. Kuna kiwanda kikubwa cha saruji. Kiwanja cha ndege kipya cha Mbeya kimejengwa hapa kwenye eneo la Bonde la Usongwe. Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 21,300 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 18,487 [2] walioishi humo. Msimbo wa posta ni 53209. Marejeo
Information related to Bonde la Songwe |