GavanaGavana (kutoka Kiingereza governor yaani "mwenye kutawala"") ni cheo cha kiongozi wa kisiasa au wa kiutawala kwenye ngazi mbalimbali. Gavana kama waziri mkuu wa jimbo katika shirikishoKuna nchi ambako gavana ni mtendaji mkuu wa serikali katika dola la shirikisho au jimbo. Kwa mfano katika Marekani ina madola 50 ndani yake na kila moja huwa na gavana kama mkuu wa serikali ya kidola. Cheo hiki kinalingana na waziri mkuu wa sehemu ya nchi yenye kiwango cha kujitawala na bunge lake pamoja na serikali ya kieneo, kwa mfano waziri mkuu wa jimbo la Afrika Kusini au Ujerumani. Gavana kama mtendaji mkuu wa mkoaKatika nchi kama Japani au Indonesia watendaji wakuu wana cheo cha gavana wakichaguliwa na wananchi na kuwajibika kwa wananchi, hata kama madaraka ya mikoa yao hayalingani na jimbo au dola la shirikisho. Katika nchi nyingine magavana ni maafisa wa serikali kuu wanaoteuliwa na rais wa taifa au waziri wake kuwa watendaji wakuu katika mkoa. Hawawajibiki kwa wananchi wa eneo lao bali kwa serikali kuu. Mfano ni gavana katika Urusi. Nafasi hii inalingana na ile ya mkuu wa mkoa katika Kenya au Tanzania tangu zipate uhuru. Gavana wa koloni na katika Jumuiya ya MadolaUgavana ulikuwa cheo cha kihistoria kutoka zamani ya ukoloni kwa mkuu wa koloni anayewakilisha serikali kuu na kuwa mkuu wa serikali katika koloni. Cheo hiki kimebaki katika Jumuiya ya Madola ambako nchi nyingi zinamkubali malkia (au mfalme) wa Uingereza kama mkuu wa dola na yeye anawakilishwa katika nchi hizo na afisa mwenye cheo cha "gavana mkuu". Gavana katika kampuni ya umma na taasisiKatika nchi zinazotumia Kiingereza kuna pia maafisa wanaoitwa gavana nje ya siasa.
Tazama pia
|