Henri IIMtakatifu Henri II (6 Mei 972 – 13 Julai 1024), alikuwa kaisari wa Dola Takatifu la Kiroma tangu tarehe 7 Juni 1002 hadi tarehe 13 Julai 1024. Ni kaisari pekee wa Ujerumani aliyetangazwa kuwa mtakatifu. Ilitokea mnamo Julai 1147 kwa tamko la Papa Klementi II. Sikukuu yake ni tarehe 13 Julai[1]. Ndoa yake na maisha ya kirohoMke wake, Kunegunda wa Luxemburg, akaja pia kutangazwa mtakatifu na Papa Inosenti III mwaka 1200. Ilisadikiwa kwamba hawakuzaa watoto kutokana na uamuzi wao wa kuishi katika ndoa kama kaka na dada kwa sababu za kidini[2]. Hakika Henri alijiunga kiroho na Wabenedikto kama mtawa wa nje. Pamoja na mkewe alishughulikia sana ustawi wa Kanisa Katoliki katika dola lake kwa kutetea haki za maaskofu na kuhimiza uaminifu wa mapadri kwa useja mtakatifu uliowapasa. Vilevile alijitahidi kueneza imani ya Kikristo kote Ulaya. Kwa ari hiyo ya kimisionari alianzisha majimbo mengi na monasteri. Angalia pia
TanbihiViungo vya nje
|