Kamerun
Kameruni, kirasmi Jamhuri ya Kameruni, ni jamhuri ya muungano katika Afrika ya Magharibi. Imepakana na Nijeria, Chadi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Gabon, Gine ya Ikweta na Ghuba ya Gine. Lugha rasmi na lugha za taifa ni Kifaransa (kinachoongoza kwa zaidi ya asilimia 80) na Kiingereza. JiografiaMaeneo kiutawalaKameruni imegawiwa katika mikoa (regions) 10 na wilaya (départements) 58. Mikoa ni:
HistoriaHistoria ya awaliKatika karne za BK Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi walianza uenezi wao kutoka huko kwenda kutawala maeneo mengi ya Afrika ya Kati, Kusini mwa Afrika na Afrika Mashariki. Wakati wa ukoloniKameruni ilikuwa koloni la Ujerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Baada ya Ujerumani kushindwa vita, nchi ikagawiwa kati ya Uingereza na Ufaransa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa kama eneo la kudhaminiwa. Tangu uhuru hadi leoMwaka wa 1960, Wafaransa waliacha Kameruni ikawa nchi huru. Wananchi wa Kameruni ya Kiingereza walipiga kura kuamua kama walitaka kuwa sehemu ya Nigeria au ya Kameruni. Kaskazini wengi walipendelea kukaa Nigeria, hivyo maeneo hayo sasa ni sehemu ya Nigeria. Wananchi wengi wa kusini waliamua wajiunge na Kameruni[4]. Kwa kusudi la kuheshimu tofauti za kiutamaduni kulikuwa na katiba mpya kwenye mwaka 1961 Shirikisho la Jamhuri ya Kameruni. Tangu 1972 muundo wa nchi ulibadilishwa kuacha mfumo wa shirikisho na kuwa jamhuri ya muungano inayokazia zaidi matumizi ya lugha ya Kifaransa ingawa Kiingereza bado ni moja ya lugha rasmi. Jina la nchi pia likabadilishwa kuwa Jamhuri ya Muungano ya Kameruni mwaka wa 1972. Hapo sehemu ya Wakamerun wanaotumia lugha ya Kiingereza walijisikia kuwa wananyimwa haki zao.[5] Baadaye, mwaka wa 1984 jina likabadilishwa tena kuwa Jamhuri ya Kameruni (kwa Kifaransa République du Cameroun). Tangu mwaka 2016 upinzani uliongezeka kati ya watu wa magharibi wanaotumia Kiingereza. Harakati hiyo ilijibiwa na serikali na polisi kwa ukali na hii umeleta kuanzishwa kwa wanamgambo wenye silaha wanaoshambulia polisi na jeshi la serikali kuu. Tangu mwaka 2017 wapinzani wamedai uhuru wa sehemu yenye lugha ya Kiingereza wakitangaza wameunda nchi mpya ya "Ambazonia". Serikali iliundwa inayokaa Nigeria; lakini kuna vikundi tofauti ambavyo wanapigana kati yao[6]. Nchi hii haitambuliwi kimataifa. Mwaka 2021 kulikuwa na majadiliano kuhusu amani kati kundi linalojiita serikali ya Ambazonia na serikali ya Kameruni[7], lakini makundi mengine yaliendelea na mapigano ya silaha[8]. SiasaUchumiWatuWakazi walikuwa 22,534,532 mwaka 2013, ambao wamegawanyika sawasawa kati ya wanaoishi mijini na wale wa vijijini. Lugha rasmi ni Kifaransa pamoja na Kiingereza. Hata hivyo wakazi wanaongea pia lugha za makabila yao mengi. Upande wa dini, 70% ni Wakristo (40% Wakatoliki na 30% Waprotestanti), 18% ni Waislamu, 3% ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika. 6% hawana dini yoyote. UtamaduniElimuTazama pia
Marejeo
Viungo vya njeSerikali
Habari
Elimu Uchambuzi
Makabila na koo
Miongozo
Utalii
|