KitigrinyaKitigrinya ( ትግርኛ, tigriññā, pia huandikwa Tigrigna, Tigrina, Tigriña; pia: Kitigray, Kitigre, Kihabesha) ni lugha ya Kisemiti inayozungumzwa katika Ethiopia (hasa jimbo la Tigray) na Eritrea. Maandishi yake ni kwa alfabeti ya Kiethiopia. WazungumzajiIdadi ya wasemaji ni takriban milioni 5-6. Wazungumzaji wa lugha hii huitwa Watigray. Nchini Ethiopia, Kitigrinya ni lugha ya tatu inayotumiwa na watu wengi (baada ya Kioromo na Kiamhari), wakati nchini Eritrea lugha hii inaongoza kuwa lugha inayotumika zaidi nchini humo. Waongeaji wengine wanaotumia lugha hii ni pamoja na wahamiaji wengi duniani ikiwa pamoja na wale wa huko Sudan, Saudi Arabia, Marekani, Ujerumani, Italia, Uingereza, Kanada na Sweden, pamoja na watu wa jamii ya Beta Israel ambao kwa sasa huishi nchini Israeli. HistoriaKitigrinya kimetokana na lugha ya kale ya Ge'ez iliyokuwa lugha ya nyanda za juu za Ethiopia na hadi leo ni lugha ya liturgia katika Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia na la Eritrea. Maandiko ya mwanzo kabisa ya lugha ya Kitigrinya yanafuata baada ya sheria za jadi zinazopatikana katika wilaya ya Logosarda, yaliyopo kusini mwa Eritrea tokea mwanzoni mwa karne ya 13.[1] Lugha ya Kitigrinya, pamoja na lugha ya Kiarabu, zilikuwa kati ya lugha rasmi katika shirikisho lililodumu kwa muda mfupi la Ethiopia na baadaye nafasi yake ilichukuliwa na lugha ya Kiamhari. Tangu kupatikana kwa uhuru wa Eritrea mwaka 1991, lugha ya Kitigrinya iliendelea kama lugha inayotumika zaidi nchini humo, na kuifanya nchi hiyo kuwa nchi pekee duniani kuitambua lugha ya Kitigrinya katika ngazi ya taifa. Katika eneo la Eritrea, wizara ya habari iliamua kuanzisha gazeti la kila wiki liandikwalo kwa lugha ya Kitigrinya lilikua likigharimu takribani senti tano na kuuza nakala zaidi ya 5,000 kila wiki. Katika kipindi hiki, gazeti hili lilifahamika kama la kipekee zaidi.[2] Lahaja za Kitigrinya hutofautiana kimatamshi, kimaana na kimaandishi.[3] Hadi sasa, hakuna lahaja ambayo imeshakubaliwa kuwa ndiyo maalum kwa watumiaji wa lugha hii. Lugha hii mara nyingi huchanganywa na lugha nyingine ambazo kwa namna fulani hufanana nazo hasa katika matamshi, kwa mfano lugha ya Kitigre ambayo lugha hii hutumika katika maeneo ya ukanda wa chini wa Eritrea, hasa upande wa Kaskazini na Magharibi ambapo lugha hii hutumika. Marejeo
Bibliografia
Viungo vya nje Kitigrinya ni toleo la Wikipedia, kamusi elezo huru
Information related to Kitigrinya |