Kiasili neno la Kilatini "Papa" linamaanisha "Baba", nalo likawa cheo kutokana na nia ya kumtaja askofu wa Roma kwa heshima ya pekee. Msingi wa heshima hiyo ni imani ya Wakatoliki kuwa askofu wa Roma ni mwandamizi wa Petro, mkuu wa mitume wa Yesu.
Wakatoliki huamini ya kwamba Petro alipewa na Yesukazi ya kuongoza Kanisa lote kwa niaba yake na ya kwamba jukumu hilo linaendelea kati ya waandamizi wa Petro kwenye kiti cha askofu wa Roma ambacho kwa heshima kinaitwa Ukulu mtakatifu.
Historia
Upapa ni kati ya vyeo vya zamani zaidi duniani na umeathiri sana historia ya binadamu kwa miaka karibu 2000.[4]Athari hiyo iliweza kuwa nzuri au mbaya, kadiri ya matendo ya mhusika.[5][6][7]
Kwa muda mrefu mamlaka ya Papa upande wa siasa, hasa juu ya mikoa ya Italia ya Kati, ilisababisha nchi nyingine na koo tajiri za Roma zijiingize katika uchaguzi ili kupitisha watu wao, hata wasiofaa. Upande mwingine, Mapapa waliathiriwa na utamaduni na mazingira ya nyakati zao, hasa tapo la Renaissance, kiasi cha kuzama katika anasa.
↑Collins, Roger. Keepers of the keys of heaven: a history of the papacy. Introduction (One of the most enduring and influential of all human institutions, (...) No one who seeks to make sense of modern issues within Christendom - or, indeed, world history - can neglect the vital shaping role of the popes.) Basic Books. 2009. ISBN 978-0-465-01195-7.
↑Faus, José Ignacio Gonzáles. "Autoridade da Verdade - Momentos Obscuros do Magistério Eclesiástico". Capítulo VIII: Os papas repartem terras - Pág.: 64-65 e Capítulo VI: O papa tem poder temporal absoluto – Pág.: 49-55. Edições Loyola. ISBN 85-15-01750-4. Embora Faus critique profundamente o poder temporal dos papas ("Mais uma vez isso salienta um dos maiores inconvenientes do status político dos sucessores de Pedro" - pág.: 64), ele também admite um papel secular positivo por parte dos papas ("Não podemos negar que intervenções papais desse gênero evitaram mais de uma guerra na Europa" - pág.: 65).
↑História das Religiões. Crenças e práticas religiosas do século XII aos nossos dias. Grandes Livros da Religião. Editora Folio. 2008. Pág.: 89, 156-157. ISBN 978-84-413-2489-3
Chadwick, Henry (1990). "The Early Christian Community". Katika John McManners (mhr.). The Oxford Illustrated History of Christianity. Oxford University Press. ISBN0-19-822928-3. {{cite encyclopedia}}: Invalid |ref=harv (help)
Franzen, August (1969). A History of the Church. Herder and Herder. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
Loomis, Louise Ropes (2006) [1916]. The Book of the Popes (Liber Pontificalis): To the Pontificate of Gregory I. Merchantville, New Jersey: Evolution Publishing. ISBN1-889758-86-8. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.