Kalisto (mwezi)Kalisto ni mwezi unaozunguka Mshtarii (Jupiter). Ni mwezi mkubwa wa pili baada ya Ganimedi unaozunguka sayari hiyo. Kipenyo chake kinalingana na kile cha sayari Utaridi (Mercury). Kati ya miezi minne mikubwa ya Mshtarii, Kalisto iko mbali zaidi na sayari hiyo ukiwa na umbali wa wastani wa km 1,889,999. Kalisto ilitambuliwa mwaka 1610 na Galileo Galilei wakati huyu alipokuwa mtu wa kwanza kutumia darubini akiangalia nyota. [1] Sawa na mwezi wa Dunia, mzunguko wa Kalisto kwenye mhimili wake unashikamana kabisa na muda wa obiti yake ("tidally locked"); kwa hiyo ni upande uleule unaoangalia sayari yake. [2] Kalisto inafanywa kwa kiwango sawa na mwamba na barafu, na densiti ya wastani ni karibu 1.83 g / cm³. Kikemia kampaundi kwenye uso ni pamoja na barafu ya maji, dioksidi kabonia, silika, na kampaundi ogania. Kipimaanga "Galileo" kilipita karibu kikafanya uchunguzi wa mwezi, na kufunua kuwa Kalisto inaweza kuwa na kiini kidogo cha silika na labda pia tabaka la maji ya kiowevu lenye unene wa zaidi ya km 100. [3] [4] Uso wa Kalisto umejaa kasoko zilizosababishwa na mapigo ya asteroidi. Hakuna dalili za michakato inayotokea chini ya uso kama vile matetemeko ya ardhi au volkeno. [5] Kalisto imezungukwa na angahewa nyembamba sana inayofanywa na dioksidi kabonia na pengine molekuli chache za oksijeni. Kuna pia tabaka la ioni (ionosphere). [6] Vipimaanga mbalimbali vimepita Kalisto, kuanzia "Pioneer 10" hadi "Galileo" na Cassini − Huygens vikapima mwezi huo. Kalisto inatazamwa kuwa mahali panapofaa kwa kuanzisha kituo kama wanadamu wanataka kufanya uchunguzi wa baadaye wa mfumo wa Mshtarii. [7] Marejeo
Maelezo ya chini |