Nabii MikaNabii Mika, ambaye jina lake la Kiebrania מיכה linamaanisha "Nani kama Mungu?", alifanya kazi ya unabii wakati mmoja na Isaya (miaka 740-700 hivi K.K.), chini ya Yotamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda. Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu, hasa tarehe 21 Desemba[1] na 14 Agosti, lakini pia 14 Januari, 18 Januari na 31 Julai[2]. UjumbeUjumbe wake unajulikana kupitia kitabu chenye jina lake katika gombo la Manabii Wadogo (Kitabu cha Mika) Humo tunasoma kwamba yeye, kama vile Isaya, alitetea haki za wanyonge (2:1-11), alipinga ibada za miungu na dhuluma pamoja na kutabiri adhabu. Lakini hasa alilitabiria taifa teule juu ya Masiya, kwamba mfalme aliyeahidiwa tangu kale atazaliwa Bethlehemu (5:1-3), tunavyosoma katika Injili ya Mathayo kuhusu uzazi wa Yesu Kristo, na kwamba atachunga Israeli kwa nguvu ya Bwana[3]. Tazama pia
TanbihiMarejeo
Viungo vya njeWikimedia Commons ina media kuhusu:
Information related to Nabii Mika |