Samia Suluhu Hassan
Samia Suluhu Hassan (alizaliwa 27 Januari 1960) ni Rais wa 6 wa Tanzania na mwanachama wa chama tawala cha Chama Cha Mapinduzi.[1] Kabla ya kuwa rais kutokana na kifo cha John Magufuli, kilichotokea tarehe 17 Machi 2021, Suluhu alikuwa makamu wa rais kwa sababu ya kuwa mgombea mwenza katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.[2] Tarehe 5 Novemba 2015 aliapishwa kama makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa mwanamke wa kwanza kufikia cheo hicho, akarudia baada ya uchaguzi mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2020. Sasa amekuwa rais wa kwanza mwanamke na rais wa Pili kutoka Zanzibar Wa kwanza Akiwa ni Ally Hassan Mwinyi Rais wa awamu ya Pili. Maisha ya awaliSuluhu alizaliwa katika Usultani wa Zanzibar. Alisoma shule za msingi za Chwaka (Unguja), Ziwani (Pemba) na Mahonda (Unguja) katika miaka ya 1966 hadi 1972. Aliendelea na masomo ya sekondari shule za Ngambo, Unguja (1973-1975) na Lumumba, Unguja (1976)[3]. Baada ya kumaliza masomo yake ya sekondari mnamo 1977, aliajiriwa na Wizara ya Mipango na Maendeleo kama karani. Alifuata kozi fupi kadhaa. Mnamo 1986, alihitimu kutoka Taasisi ya Usimamizi wa Maendeleo (Chuo Kikuu cha Mzumbe cha leo) na diploma ya hali ya juu katika utawala wa umma. [4] Baada ya kuhitimu, aliajiriwa kwenye mradi uliofadhiliwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (World Food Programme). Kati ya miaka 1992 na 1994, alisoma kwenye Chuo Kikuu cha Manchester, Uingereza na kuhitimu stashahada ya uzamili katika uchumi. [5] Mnamo mwaka 2015, alipata MSc yake katika Maendeleo ya Uchumi wa Jamii kupitia mpango wa pamoja kati ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na Chuo Kikuu cha Kusini mwa New Hampshire. [6] Kazi ya siasaMnamo mwaka 2000 aliamua kujiunga na siasa. Aliteuliwa na CCM kama mbunge wa viti maalum katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar akateuliwa na rais Amani Karume kuwa waziri wa utalii na bishara. Alikuwa mwanamke pekee kwenye ngazi ya mawaziri akaona alidharauliwa na wenzake wa kiume kwa sababu ya jinsia yake. [7] Alichaguliwa tena mnamo 2005 kwenye viti maalum na aliteuliwa tena kama waziri katika wizara ya kazi, jinsia na watoto. [8] Mwaka 2010 aligombea kwenye uchaguzi kwa Bunge la Kitaifa, akisimama katika jimbo la Makunduchi na kushinda kwa zaidi ya % 80. [9] Rais Jakaya Kikwete alimteua kuwa Waziri wa Nchi wa Mambo ya Muungano. [10] Mnamo 2014, alichaguliwa kama Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba iliyokuwa na jukumu la kuandaa katiba mpya ya nchi. [11] Mnamo tarehe 30 Aprili 2021 alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa CCM [12] akiwa mwenyekiti wa kwanza mwanamke. Makamu wa RaisMnamo Julai 2015, mteule wa urais wa CCM, John Magufuli alimchagua kuwa mgombea mwenza wa uchaguzi wa 2015 na kumfanya kuwa mgombea mwenza wa kwanza mwanamke katika historia ya chama hicho. [13] Baadaye alikuwa makamu wa rais wa kwanza mwanamke katika historia ya nchi kutokana na ushindi wa Magufuli katika uchaguzi. [14] Maisha ya binafsiMnamo 1978 aliolewa na Hafidh Ameir aliye kwa sasa afisa kilimo mstaafu. Wana watoto wanne: binti mmoja na wavulana watatu. [15] Binti yake Wanu Hafidh Ameir (aliyezaliwa 9 Februari 1982), mtoto wa pili, ni mbunge wa viti maalum katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar. [16] Tanbihi
|